Daru Rasuulul A’adham (s.a.w.w) yafanya nadwa ya pili na yaweka mezani mjadala wa Almaghaazi ya kwanza na mwandishi wake…

Maoni katika picha
Daru Rasuulul A’adham (s.a.w.w) katika kituo cha (Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat) kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa harakati zake za mambo ya kihistoria, imeandaa nadwa ya kielimu yenye anuani isemayo: (Miongoni mwa waandishi wa Almaghaazi ya kwanza ni Abbaan bun Othumani Ahmar Albajalliy aliye fariki mwaka wa 170 hijiriyya), nadwa hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa mikutano katika kituo cha kimataifa Al-Ameed.

Mtowa mada katika nadwa hiyo alikua ni mkuu wa kitivo cha lugha kutoka Jamiatu Al-Iraqiyya Dokta Hussein Dakhili Bahadeli, muhadhara wake ulijikita katika kuelezea mambo yaliyo fanywa na Abbaan bun Othumani yanayo husu historia ya Mtume, na uhusiano uliopo baina yake na Abbaan bun Othumani bun Affaan.

Bahadeli alisema kua: “Mada iliyopo mbele yetu inahusu mmoja wa wapokezi wa hadithi wa mwanzo kabisa wa kishia, na historia ya Mtume pamoja na Almaghaazi kwa upande mwingine, mpokezi huyo ni Abbaan bun Ahmar Albajaliy aliye fariki mwaka wa (170h), mpokezi aliye potezwa na historia na kufutwa athari yake, bali sifa zake akapewa mpokezi mwingine kwa sababu tu ya kufanana majina yao, ambaye ni Abbaan bun Othumani bun Affaan aliye fariki mwaka wa (105h). nitajaribu kuongea baina ya majina hayo mawili ili tumpe kila mmoja haki yake kama alivyo julikana, pia utafiti wangu haukujikita katika kulinganisha ubora wao hadi tubaini yupi mbora zaidi katika sekta hii, sekta ya historia ya Mtume, japokua nitamzungumzia zaidi Abbaan bun Othumani Ahmar Albajaliy”.

Akaongeza kua: “Katika kusoma maisha ya Abbaan Albajaliy na historia yake ya kielimu pamoja na kuzaliwa kwake kuna walio mnasibisha na kundi la Nausiyya, ambalo ni moja ya vikundi vya shia lililo kua linaamini kua Imamu Swadiq (a.s) hakufariki na yeye ndiye Mahdi, pamoja na kua utafiti umekanusha habari hiyo, pia huyu ni miongoni mwa waandishi wa kwanza wa historia na ndiye aliye andika kitabu cha Almaghaazi”.

Mwishoni mwa nadwa hii inayozingatiwa kuwa miongoni mwa nadwa za kielimu zinazo ratibiwa na Daru Rasuulul A’adham (s.a.w.w), kulikua na maoni, maswali na michango mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, mtowa mada alijibu maswali na kufafanua pale palipo hitaji ufafanuzi zaidi, na mwisho kabisa vikatolewa vyeti vya ushiriki kwa kila mshiriki wa nadwa hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: