Vituo vya Ashura: Mwezi kumi na tisa Muharam mateka wa Imamu Hussein (a.s) walitoka Kufa na kwenda Sham…

Maoni katika picha
Watu wa Imamu Hussein (a.s) walio tekwa walipitia mazingira mengi magumu, katika siku kama ya leo mwezi kumi na tisa Muharam mwaka (61) hijiriyya, msafara wa mateka uliondoka Kufa na kwenda Sham wakitanguliwa na vichwa vya mashahidi, na mbele kabisa kikiwa ni kichwa cha Imamu Hussein (a.s), baada ya Yazidi kumuandikia barua gavana wake wa Kufa Ubaidullahi bun Ziyadi, ya kumtaka awapeleke kwake, barua hiyo ilikua inasema: (Walete mateka kwangu), alitaka kuifurahisha nafsi yake ovu, kwa kuiona familia ya Mtume (s.a.w.w) ikiwa mbele yake huku wamefungwa minyororo, Ibun Ziyadi akamwita Mafkharu bun Tha’alaba Al’Aaidhiy, akamkabidhi vichwa vya mashahidi pamoja na mateka ambao ni watu wa familia ya Mtume (a.s), akamuamrisha yeye pamoja na Shimri bun Dhijaushen wawapeleke kwa Yazidi katika huko Sham.

Msafara wa mateka ukaondoka katika mji wa Kufa na kuelekea Sham ukiwa umetanguliwa na vichwa vya mashahidi ambavyo miili yao ilibaki katika jangwa la Twafu, na mbele kabisa wakitanguliwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s), nyuma ya vichwa wakapangwa wanawake na watoto, wakitanguliwa na bibi Zainabu (a.s) jemedari wa Karbala, naye ndiye aliye beba jukumu la kuongoza harakati ya Imamu Hussein dhidi ya matwaghuti, nalo ni jukumu la jihadi ya kutumia maneno na sio upanga, alitekeleza jukumu hilo pamoja na mtoto wa kaka yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s) ambaye mikono yake ilifungwa minyororo na kuwekwa shingoni kwake, walipandishwa juu ya migongo ya ngamia isiyo kua na tandiko wala mwamvuli, (Ni safari isiyokua na maandalizi, ngamia hazikua na matandiko wala hawakua na vitambaa au vitu vingine vya kuweka kwenye migongo ya ngamia) msafara uliendelea kukata masafa wakielekea Damascus.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: