Kwa ushiriki wa watu (130): Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua hatua ya tatu ya kongamano la Qamaru Thaqafi…

Maoni katika picha
Kongamano la Qamaru Thaqafi la kielimu linalenga tabaka tofauti za watu katika jamii, na linakusudia kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, kwa kutumia njia za kisasa zisizo kua na chuki wala uhasama unao weza kuleta madhara katika jamii.

Ukizingatia mambo yaliyo fanikishwa na kongamano hili linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, katika awamu za nyuma ziliyo husisha mkoa wa Dhiqaar na Baabil, tumeingia katika awamu ya tatu yenye jumla ya washiriki (130) kutoka mkoa wa Misaani na Muthana, ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu na watumishi wa elimu na watu wa sekta zingine, kongamano hili linafanyika ndani ya jengo la Shekh Kuleini lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kongamano litadumu siku saba, na linaratiba ya mihadhara na majadiliano yanayo lenga kuandaa viongozi na kupambana na mmomonyoko wa maadili na upotoshaji wa vyombo vya habari pamoja na kurekebisha nafsi, sambamba na mihadhara ya Aqida na masomo mbalimbali ya kiislamu, inayo tolewa na jopo la maustadhi walio bobea katika fani hizo.

Ustadh Ali Badri ambaye ni mmoja wa wahadhiri katika kongamano hilo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Raia wa Iraq wanashambuliwa na mmomonyoko wa maadili, unao lenga kuondoa uzalendo wa mwananchi na kuharibu imani ya dini, kupitia upotoshaji wa vyombo vya habari na kusambaza fikra zinazo haribu amani ya jamii, makongamano haya yanawawezesha washiriki kuchuja habari na kuwaandaa kuwa watu muhimu katika jamii watakao weza kupambana na fikra potofu ndani ya jamii zetu”.

Akaongeza kua: “Tuna imani kubwa na washiriki wa kongamano, tunatarajia kongamano hili liwe na matunda mazuri kama yalivyo kua makongamano yaliyo pita katika mikoa mingine, tumeona hamasa kubwa kwa washiriki baada ya kupewa mada zinazo elezea mazingira halisi wanayoishi vijana wa siku hizi”.

Kumbuka kua semina nyingi za kitamaduni na warsha mbalimbali hufanywa na vijana wanapo maliza mafunzo katika (kongamano la Qamaru Thaqafi) yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo yanamchango mgubwa na muhimu katika kuandaa vijana wenye uwelewa na uwezo wa kubeba majukumu ya kidini na kitaifa kwa ajili ya kupambana na changamo za kiutamaduni zisizo kuwa na mwisho kama zilivyo vita vya kutumia siraha, Atabatu Abbasiyya pamoja na kuandaa ratiba na wahadhiri, inagharamia usafiri, malazi na chakula pamoja na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: