Mwenyezi Mungu aliutukuza uislamu kwa kuweka Maimamu watakatifu walioihami Dini kwa kila kitu wanacho miliki, wakafanya kila wawezalo kwa ajili ya kuifanya Dunia iwe na amani na utulivu, walipo fariki Mwenyezi Mungu kawaleta watu walio waamini na kuwatii Maimamu na wakafuata mwenendo wao bila kuogopa mauti, na kuifanya fikra ya Ahlulbait (a.s) kua endelevu katika uhai wote.
Miongoni mwa mashahidi watukufu walio kirimiwa rehma na maghfira kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu mtukufu ni jemedari wetu (Maahir Ali Rahim Aljuburi), naye ni miongoni mwa wale walio tekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu naye atawaingiza peponi, kwa kauli yake isemayo: (Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao kwa wao watapata pepo, wanapigana katika njia ya Mwenyezi Ngungu wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa haki katika Taurati na Injili na Qur’ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndio kufuzu kukubwa), kutokana na alivyo jitolea kwa ajili ya Dini yake, heshima yake na maeneo matukufu.
Alizaliwa katika mji wa Karbala (18/02/1974m), katika familiya iliyokua inapeperusha bendera ya Imamu Hussein (a.s) juu ya nyumba yao, alijulikana kwa kushikamana kwake na misingi ya kiislamu pamoja na fikra za Ahlulbait (a.s) na uwelewa wa mipaka ya Mwenyezi Mungu mtukufu, alikulia katika mji wa Karbala na akasoma elimu ya msingi na sekondari katika mji huo, akanywa maji ya ubinadamu na upole, alikua anapenda kufanya mambo ya heri na alipendwa na kila mtu, alikuwa mtu wa pekee katika jamii, aliipenda sana kazi yake pale alipo jitolea kuwa miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kitengo cha mitambo (magari), jambo lililo pelekea viongozi wa idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu kumlipa sawa na wenzie, kutokana na utendaji wake, uongozi ukamthibitisha kuwa mfanyakazi rasmi tarehe (24/08/2013m).
Baada ya kutolewa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda na Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, alionyesha azma yake iliyo tokana na imani yake ya Husseiniyya, akajiunga katika safu ya watu wanaojitolea katika kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), akashiriki vita ya ukombozi katika maeneo mengi, akawa anabeba wapiganaji kwa kuwasiliana na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kutoka katika miji mbalimbali ya Iraq na kuwapeleka katika maeneo ya vita na kuwarudisha, bila malipo yeyote pamoja kua kazi hiyo ilihitaji nguvu nyingi, kila safari alikua anatumia siku kumi hadi kumi na tano na zaidi, wakati mwingine msafara wake ulikua unapita katika maeneo yenye vita kali, kutokana na dharura ya kuhakikisha vita haisimami, pamoja na kazi hiyo akaamua kuwa mpiganaji rasmi katika uwanja wa vita japo kua viongozi wake walimkatalia kwa kipindi fulani.
Alipigana katika maeneo mengi na akapata utukufu wa shahada katika vita ya kukomboa mji wa Bashiri tarehe (10/04/ 2016m), mwili wake pamoja na miili ya mashahidi wengine haikupatikana katika uwanja wa vita, ulikuja kupatikana baadae kabisa katika eneo la karibu na mji wa Huweija, Mwenyezi Mungu akurehemu ewe mpiganaji shujaa na akuweke mahala pema peponi.