Uongozi maalumu wa Mazaru ya swahaba mtukufu Salmaani Muhammadiy (r.a) wafanya majlis ya kuomboleza katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya…

Maoni katika picha
Kama desturi yake katika siku kama hizi za huzuni, uongozi mkuu wa mazaru ya swahaba mtukufu Salmaani Muhammadiy (r.a) na maukibu ya Answaru Sayyidat Ruqayya (a.s) katika mji wa Madaaini wamefanya majlisi kubwa ya kuomboleza, katika malalo matukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhuisha na kukumbuka tukio la Twafu.

Waombolezaji walisimama kwa mistari na walianzia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), majlisi hiyo ilihusisha uimbaji wa kaswida na upigaji wa matam zilizo amsha hisia za majonzi kutokana na yale yaliyo wafika watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika siku kama hizi, kwa kuuwawa, kunyanyaswa na kuchomewa mahema na mengineyo mengi miongoni mwa jinai za kibinadamu, kisha waombolezaji wakelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kufanya kama walivyo fanya ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bado zinaendelea kupokea mawakibu za waombolezaji wa Husseiniyya kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kuna mawakibu ambazo zinakuja kutoa pole kwa kufuata muda walio pangiwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ndani ya kumi la kwanza, la pili au la tatu katika mwezi mtukufu wa Muharam, huendelea namna hiyo hadi mwisho wa mwezi wa Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: