Asubuhi ya leo (20 Muharam 1440h) sawa na (30 Septemba 2018m) shule za Al-Ameed zimepokea mamia ya wanafunzi wa ngazi tofauti katika vituo vyake vyote, ikiwa ni mwanzo wa muhula mpya wa masomo huku wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mwaka huu kama walivyo fanya katika miaka iliyo pita.
Rais wa kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Didah ameonyesha furaha kubwa baada ya kuona hamasa ya wanafunzi tangu siku ya kwanza ya mwaka mpya wa masomo, akabainisha kua: “Tunajitahidi kumnufaisha kila mtoto kadri ya uwezo wetu, kwa kuwapa elimu na malezi bora kwa mujibu wa malengo ya uwanzishwaji wa kituo hiki, kwa kufuata mfumo wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambao umeanza kuonyesha matunda yake mwaka baada ya mwaka”.
Akabainisha kua: “Hakika tumefanya kila kilicho ndani ya uwezo wetu kwa ajili ya kutoa malezi na elimu bora itakayo saidia jamii yetu na jamii zingine, mwaka huu tumefungua shule mbili mpya na moja ya awali na kuziingiza rasmi katika orodha ya vitengo vyetu vya elimu, pamoja na kuendesha masomo ya muda mfupi kwenye vipindi vya likizo kwa lengo la kuongeza kiwango cha elimu na kukuza vipaji chini ya utaratibu bora unaotumiwa na nchi zilizo endelea, kiu yetu kubwa ni kuhakikisha tunamwandaa mwanafunzi kielimu na kumwezesha kuwa nyenzo muhimu ya maendeleo, mwisho tunategemea mwaka huu shule na vyuo vyetu vifanye vizuri na kufurahisha nyoyo zetu”.
Didah akaendelea kusema kua: “Hakika shule zetu zimeanza kutekeleza mradi wa (Wiki ya kuishi kwa amani) unao lenga kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza ambao mazingira ya shule bado ni mageni kwao, mradi huo unavipengele vingi, tunawapa zawadi na michezo ya kimasomo kwa ajili ya kuwashajihisha na kuwafanya wapende kusoma, pia tunawaonyesha filamu maalumu za katuni, sambamba na kuwapa nasaha na maelekezo mbalimbali, kwa ajili ya kuondoa mazingira ya hofu na uwoga kwa wanafunzi na kuhakikisha mazingira ya shule yanawawezesha kuonyesha uwezo na vipaji vyao”.
Wazazi wameonyesha furaha kubwa kutokana na uratibu mzuri walio uwona, na maandalizi ya idara za shule katika kuwapokea watoto wao pamoja na mazingira mazuri ya walimu ambao unaonekana uwajibikaji wa ulezi bora kwa watoto wao.
Kumbuka kua shule za Al-Ameed zimezowea kufanya mahafali maalumu za ufunguzi wa shule kila mwaka, lakini kutokana na mwaka huu kuangukia katika mwezi wa Muharam hawajafanya mahafali, wametosheka na kufanya mkutano wa asubuhi, ambao wametoa nasaha na maelekezo kwa wanafunzi pamoja na kuwahimiza waongeze juhudi katika masomo.