Kazi ya kuweka maandishi ya Qur’ani yaliyo tengenezwa kwa dhahabu katika eneo kubwa lililowekwa dhahabu kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeanza…

Maoni katika picha
Ukamilishaji wa mradi wa ujenzi na uwekaji wa dhahabu katika sehemu ya jengo la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mafundi na wahandisi wameanza kazi ya kuweka maandishi ya Qur’ani yanayo kaa katikati ya upande wa ukuta wa ndani katika sehemu ya dhahabu ijulikananyo kama (Twarima).

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ambaye alisema kua: “Hakika lengo la kutekelezwa mradi huu, ambao unazingatiwa kuwa mradi muhimu sana kutokana na nafasi yake kiroho, kwa nini isiwe hivyo wakati ndio mlango wa kuingia katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na baada ya kukamilika kwa kiasi kikubwa uwekaji wa vifuniko vya dhahabu katika eneo kubwa linalo julikana kama (Twarima) kwa ndani, sehemu hiyo kazi ilianzia chini kwenda juu, sasa hivi tumefika sehemu muhimu sana, ambayo ni sehemu ya kuweka maandishi ya Qur’ani ambayo yapo katikati ya Twarima, maandishi yaliyo tengenezwa kwa umaridadi wa hali ya juu na kutiwa nakshi zinazo endana na utukufu wa jengo hili”.

Akabainisha kua: “Hakika maandishi ya Qur’ani yatawekwa pande tatu, ili zaairu (mtu) aweze kusoma kwa urahisi, sambamba na kulinda muendelezo wa maneno, ambayo yanasifa zifuatazo:

  • - Aina ya hati iliyo tumika katika maandishi hayo ni Thuluthul-Jalliy yenye ujazo na imetiwa dhahabu ya iyaar (kipimo) (24), ambayo inaviwango vya aina tatu; na ukubwa wa (sm 3.6), kazi hiyo ilifanywa na mtaalamu wa hati wa kiiraq Ustadh Farasi Abbasi.
  • - Upande wa kulia unaukubwa wa (sm 351 x sm 80) na umeandikwa surat Ikhlasi.
  • - Upande wa katikati unaukubwa wa (sm 700 x sm 80) umeandikwa sehemu ya aya ya 177 iliyopo katika surat Baqarah.
  • - Upande wa kushoto unaukubwa wa (sm 349 x sm 80) umeandikwa surat Kauthar (Innaa a’twainaakal-kauthar..).
  • - Jumla ya vipande vitatu vya maandishi ni (sm 80 x 14 mt)
  • - Vipande vya maandishi vimewekwa dhahabu halisi na vimetiwa Mina ya bluu.
  • - Maandishi hayo yamezungukwa na mapambo mazuri ya kiislamu kwa juu yenye ukubwa wa (sm 20) na kwa chini kiwango hicho hicho, na yametiwa dhahabu iyaar (kipimo) (24).

Kumbuka kua hatua hii inakamilisha hatua zilizo tangulia za kuweka marumaru katika nguzo za Twarima na ubavuni mwake, na itapendezesha zaidi uzuri wa Ataba tukufu, pia inatunza uzuri wa muonekano wake kwa muda mrefu, pamoja na kuhifadhi uasili wa jengo na urithi wake katika ubora wa hali ya juu kabisa, na kwa viwango vya kiufundi na kiuhandisi vilivyo pasishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: