Kwa mara ya kwanza katika historia ya Ataba tukufu za Iraq: Atabatu Abbasiyya yajiandaa kufanya kongamano lake katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zake za ndani na nje, Atabatu Abbasiyya tukufu inajiandaa kuratibu na kushiriki katika tukio muhimu kimataifa ambalo ni kongamano la (Kurudisha nafasi muhimu na kuzipa nguvu jamii adilifu na kueneza amani), kwa kushirikiana na taasisi ya Imamu Khui na umoja wa kielimu wa utafiti na turathi.

Kongamano litafanyika tarehe nane ya mwezi huu wa Oktoba, linatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya (1000) wa Dini na tabaka tofauti.

Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu ni sawa na Ataba zingine ina nafasi ya ubaba kwa waislamu wote, hasa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wa mielekeo yote. Vilevile ni kimbilio la nyoyo za watu wote bila kujali tofauti za Dini zao, kwa sababu ni shule ya ushujaa, kujitolea, kuunga undugu na uaminifu, ni shule ambayo imefundisha Dunia kwa zama na zama namna ya kujitolea kwa ajili ya kulinda haki isiharibiwe, na kuzuia badili isitawale.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi yake ya utamaduni na elimu, imekua ikifanya kazi kwa mlengo wa uwadilifu na msimamo wa kati, ili iweze kuzuwia mashambulizi ya wakufurishazi wanao shambulia umma wa kiislamu, na kupambana na fikra potofu katika jamii ya kiislamu, wamesha fanya makongamano mengi na harakati mbali mbali ndani na nje ya Iraq kwa ajili ya kulingania mwenendo huo na kuufundisha katika jamii ya raia wa Iraq na duniani kwa ujumla. Kongamano hilo linalenga kuwakutanisha wasomi mbalimbali duniani na kubaini fursa pamoja na kuangalia changamoto zinazo ukabili umma wa kiislamu na kuangalia namna ya kuurejesha uislamu katika nafasi yake kimataifa.

Mapendekezo yote yatajadiliwa katika kongamano hilo kupitia kifungu (namba 16 cha SDG) jamii adilifu na amani na utulivu katika jamii za kiislamu, kwa ajili ya kuzuia ukatili kwa makundi ya wachache pamoja na kuchambua kifungu (namba 5 cha SDG) kinacho husu wanawake na watoto na kifungu (namba 17 cha SDG) vifungu hivyo ni vya umoja wa mataifa kuhusu maendeleo endelevu ambayo yanatarajiwa kufikiwa kwa ukamilifu mwaka (2030) yapo malengo (17), kongamano hilo litasaidia kuuonyesha uislamu kama mshirika muhimu katika kutatua changamoto nyingi zinazo ukabili ulimwengu, na litawapa moyo waislamu kufanya tafiti za kisekula.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati inayo simamia maandalizi ya kushiriki katika kongamano hilo: “Atabatu Abbasiyya tukufu itapata nafasi ya kuzungumza na itapewa nafasi ya kuonyesha picha za mnato kwa jina la (Utamaduni wa Iraq) picha hizo zitaonyesha athari ya uharibifu uliofanyika Iraq na namna turathi na utamaduni alivyo haribiwa na magaidi wa Daesh, pamoja na kuonyesha msimamo na ushujaa wa raia wa Iraq walio simama imara kupigana na Daesh na wakawashinda kwa kipindi kifupi, na sasa hivi wanajenga upya nchi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: