Mwaka wa tano mfululizo: Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya visomo vya Sajjaadiyya…

Maoni katika picha
Mwaka wa tano mfululizo Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikishiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya usomaji wa Sajjaadiyya, yaliyo funguliwa Juma Tatu asubuhi (21 Muharam 1440h) sawa na (1 Oktoba 2018m) na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahdi Karbalai katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, chini ya ushiriki wa vituo vingi vya usambazaji wa vitabu vya hapa Iraq na kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi pamoja na matawi ya Ataba tukufu, maonyesho haya ni miongoni mwa shughuli za kongamano la visomo vya Sajjaadiyya la kimataifa litakalo anza siku ya Ijumaa ijayo linalo fungamana na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s), hambalo huandaliwa na kusimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya inawakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni pamoja na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, ambapo kitengo cha kwanza kimesheheni machapisho mbalimbali, vitabu na cd za mafundisho ya Dini, Akhlaqi, Malezi, pamoja na mafundisho ya sekula, na vitabu vingine vilivyo fanyiwa uhakiki na kuchapishwa katika muonekano mpya, tena vitabu vinavyo lenga rika za aina zoto.

Kuhusu kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, pia kimesheheni machapisho ya kitengo hicho na machapisho ya vituo vilivyo chini yake kama vile (kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, na kituo cha turathi za Basra), pamoja na chapisho la Qur’an tukufu lililofanywa na Maahadi ya Qur’ani ikiwa ni pamoja na msahafu ulio chapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano Sayyid Jamali-Dini Shahristani amebainisha kua: “Hakika vikundi vya usambazaji wa vitabu (76) vinashiriki katika maonyesho haya, kutoka katika nchi za Tunisia, Moroco, Misri, Lebanon, Uturuki, Iraq, Omani, Sirya na Iran, wakiwa na zaidi ya vitabu elfu (25)”, akazungumzia uwepo wa nchi ya Moroco katika maonyesho haya akasema kua: “ Hikika maonyesho haya yamepanua wigo zaidi kwani maonyesho yaliyo tangulia yalikua yanahusisha nchi za mashariki ya kati peke yake”.

Tunapenda kukumbusha kua kongamano la (visomo vya Sajjaadiyya) linasimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa mwaka wa tano mfululizo linalenga kumuelezea Imamu Zainul-Aabidina (a.s) hasa kuifafanua Risalatu Huquuqi kwa sababu imeanza kusahaulika, pembezoni mwa kongamano hufanyika maonyesho ya vitabu ambayo huhusishwa vituo vingi zaidi vya usambazaji wa vitabu vya kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: