Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) yazindua App ya (Haqibatu Zaairu)…

Maoni katika picha
Kutokana na kuingia mwezi wa huzuni, mwezi wa Muharam na ujio wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na kwa ajili ya kunufaika na teknolojia ya mitandao ya kielektronik na kuhakikisha inatumika vizuri na kuhudumia jamii kubwa zaidi, kufuatia pia maendeleo ya kisasa, kituo cha habari Alqamaru kilicho chini ya Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao ya Atabatu Abbasiyya tukufu imezundua App iitwayo (Haqibatu Zaairu).

App hii inafanya kazi katika simu za kisasa (smart phone) zenye uwezo wa (Angroid) kupitia anuani ya: https://play.google.com/store/apps/details?id=alanbiaaturath.apps.visitorbag

Na inakila kitu anachohitaji zaairu awapo ziarani katika malalo matukufu, kwenye siku za matukio maalumu na zinginezo, App hiyo inakurasa nyingi na unaweza kuzisoma kwa urahisi, nazo ni:

 • 1- Mwongozo wa majlisi za Husseiniyya: nao ni ukurasa maalumu wa watu wenye mawakibu kwa ajili ya kuonyesha sehemu na muda wa majlisi ya Husseiniyya na minasaba mingine ya Dini kwa mazuwaru wote. Na kuna uwezekano wa:
 • a- Kuweka tangazo la (maukibu au kikundi) la majlisi au mnasaba pamoja na kuelezea sehemu ya tukio na muda.
 • b- Uwanja wa matangazo na uwezekano wa kutafuta kwa njia rahisi itakayo muwezesha mtumiaji kufahamu majlisi ya karibu na sehemu alipo.
 • c- Uwanja maalumu wenye maelezo kwa ufupi kuhusi minasaba na utukufu wake.
 • 2- Ziara za Maimamu watakasifu (a.s) na dua zilizo pokelewa: ukurasa huu unamuwezesha mtumiaji kusoma au kusikiliza dua na ziara zinazo husiana na minasaba mbalimbali.
 • 3- Kituo cha walio potea na vilivyo potezwa: ukurasa huu unahusika na kutangaza watu waliopotea au vitu vilivyo potea ili kusaidia kupatikana kwa urahisi.
 • 4- Mwongozo wa njia: ukurasa huu unamuonyesha mtumiaji vituo muhimu na sehemu zinazo toa huduma kupitia njia ya (Yaa Hussein), pamoja na mambo yafuatayo:
 • a- Kuonyesha mchoro wa barabara na kubainisha sehemu muhimu.
 • b- Kiwango cha umbali na muda anaoweza kutumia kufika sehemu anayo kusudia.
 • 5- Mwongozo wa kukaribisha mazuwaru: ukurasa huu unamsaidia mtumiaji kufahamu sehemu za malazi ya bure, au matangazo kuhusu sehemu zinazo pokea mazuwaru katika minasaba ya Dini na katika siku za kawaida, pamoja na uwezekano wa:
 • a- Tangazo la nyumba inayo laza watu bure, pamoja na kuelekeza mahala ilipo na ukubwa wake, na kubainisha muda wa huduma hiyo na mengineyo.
 • b- Tangazo litawekwa baada ya kukubalika na kupasishwa na idara.
 • c- Uwanja wa kuangalia nyumba zilizopo kwa ajili ya makazi ya mazuwaru na uwezekano wa kutafuta kulingana na mji ulipo au ukubwa wa nyumba.
 • 6- Fiqhu Zaairu: ukurasa huu unamaswali na majibu ya kifiqhi maalumu kuhusu zaairu kutokana na eneo lake.

Na kuna uwezekano wa kutuma swali na litajibiwa na kamati maalumu iliyopewa jukumu hilo.

Kumbuka kua Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imesha tengeneza App kadhaa zinazo fanya kazi katika simu za kisasa (smart phone) zenye uwezo wa (Android) na (ios).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: