Nyota zinazo ng’aa angani hudondoka moja moja pale zinapo tumika kupiga shetani, hakika ni taa za mbinguni na mwanga wake huangaza bila mipaka, hali kadhalika mashahidi ni taa za ardhini wapo sawa na nyota huanguka mmoja mmoja wanapo washambulia mashetani wa ardhini, watu wenye fikra potofu na ugaidi kama wale walio jikusanya chini ya bendera ya Daesh, hakika mashahidi hukumbukwa milele, na miili yao hufunikwa bendera ya taifa lao kama ishara ya utukufu wao, miongoni mwa nyota tukufu za mashahidi wetu ni Ahmadi Maliki Al-Aaridhiy, mmoja wa mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.
Alikua anafanya kazi katika mji mtukufu wa Karbala, akiwa mmoja wa watumishi wa Imamu Hussein (a.s) katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, idara ya nidham kuanzia tarehe (14/06/2008), alizaliwa katika mkoa wa Samawah 18/09/1977), amelelewa na kukulia katika mji huo ndani ya familia inayo julikana mapenzi yao na ufuasi wao kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na ikhlasi yao katika kufuata mwenendo mtukufu uliowekwa mizizi kwa damu ya bwana wa mashahidi (a.s), hakupenda kuishi mbali na bwana wa mashahidi (a.s), akahama yeye pamoja na familia yake wakaja katika mji wa Karbala ili aishi jirani na Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Shahidi alikua na sifa nzuri, marafiki wake na kila aliye ishi naye anashuhudia uzuri wake, alikua na roho nzuri anaye penda kufanya kheri, alifanya mambo yanayo mridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Ahlubait wake, marafiki zake na majirani zake wamesema kuwa: Hakika alikua hamuudhi yeyote wala hamkasirikii anaye muudhi hamsemi vibaya wala hamfanyii mabaya, alikua na tabia njema mwenye uhusiano mzuri na marafiki zake pamoja na wafanya kazi wenzake, alikua mnyenyekevu sana anapo amiliana na mazuwaru wanao kuja katika mji wa Karbala, alijiunga katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji baada ya kutolewa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda, na ameshiriki kwenye mapigano mengi dhidi ya magaidi wa Daesh, pamoja na kazi yake ya kutoa huduma na kupigana jihadi, alijiunga vilevile na kikosi maalumu cha kutengeneza siraha kubwa na ndogo akiwa katika uwanja wa vita kwa vitengo, hakwenda kusomea sehemu salama zilizo mbali na mapigano, alipata utukufu wa shahada pamoja na watukufu wengine katika vita ya mwisho ya kukomboa mji wa Mosul kwenye opreshen ya (tunakuja ewe Nainawa) tarehe 14/12/2017m ambayo ilikua ni vita kali zaidi, ilikuwa ni sehemu ambayo magaidi wote walikusanyika hapo na wakajiandaa vizuri kukabiliana na jeshi la serikali bamoja na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, hapo zilianguka nyota tukufu za mashahidi na damu zao zikatengeneza daraja la ushindi, miongoni mwao ni Shahidi Ahmadi Maliki Al-Aaridhiy, amani iwe juu yake na rehma milele na milele.