Atabatu Abbasiyya tukufu yakusudia kuadhimisha wiki ya utamaduni nchini Ujerumani…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imekusudia kuadhimisha wiki ya kitamaduni nchini Ujerumani kwa jina la (Wiki ya Abulfadhil Abbasi –a.s-), maadhimisho hayo yataanza tarehe nane mwezi huu na yatakuwa na vipengele tofauti katika miji mitatu ya Ujerumani ambayo ni Gotagen, Balin na Frankford.

Mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa Ulaya Sayyid Ahmadi Raadhiy Alhusseiniy ametuambia kua: “Wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni moja ya maadhimisho yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya ndani na nje ya Iraq, na yamekua na mafanikio makubwa sawa sawa na maadhimisho ya (Hema la Ashura) yanayo fanyika Uturuki na (kongamano la Amirul Mu-uminina) linalo fanyika India na maadhimisho ya wiki ya utamaduni yanayo fanyika Iran na Pakistani, kwa hiyo maadhimisho haya ni sehemu ya kuendeleza mafanikio yaliyo fikiwa, na nchi ya Ujerumani ndio mwenyeji wa maadhimisho ya mwaka huu ambayo huwa na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni:

  • - Kufanya kongamano la kitafiti katika chuo kikuu cha Gotagen chini ya anuani isemayo: (Elimu za kiislamu na mafundisho yake baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Gotagen), chini ya uhadhiri wa watafiti wa Iraq na Ujerumani watakao wasilisha mada mbalimbali, kama vile; kuvumiliana na kuishi kwa amani, kumkubali mwenzako, mazungumzo baina ya wana Dini tofauti, tafiti hizo zitakua na mitazamo ya kihauza na kisekula na kongamano litachukua siku tatu.
  • - Nadwa maalumu kuhusu Atabatu Abbasiyya tukufu itakayo ilezea huduma zinazo tolewa na Ataba tukufu kwa mazuwaru na wengineo miongoni mwa jamii za wairaq, na kuelezea miradi mikubwa inayo fanywa na Ataba ya ujenzi na elimu.
  • - Kutembelea taasisi za dini katika miji hiyo (tajwa hapo juu).
  • - Kushiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yatakayo fanyika katika jiji la Frankford, Atabatu Abbasiyya tukufu itashiriki kupitia machapisho yake ya kitamaduni na kielimu, ushiriki huu ni muhimu kwake, kwani maonyesho haya ni moja ya njia za kujitangaza kimataifa na fursa ya kutambulisha mafanikio yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: