Kongamano la kitamaduni Alqamaru lahitimisha awamu yake ya tatu…

Maoni katika picha
Kongamano linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu la Alqamaru limehitimisha awamu yake ya tatu, iliyo kua na washiriki (150) kutoka katika mkoa wa Misaan na Muthanna, hafla ya ufungaji wa kongamano hilo ilipata mahudhurio makubwa na ilifanyika katika ukumbi wa jengo ya Shekh Kuleini siku ya Juma Tatu (21 Muharam 1440h) sawa na (1 Oktoba 2018m), hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na mmoja wa washiriki bwana Mahdi Hussein, halafu ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa kwa niaba na Shekh Haarith Daahi, ambaye alisema kua: “Semina na makongamano ya vijana yana umuhimu mkubwa; yanawafundisha tamaduni nzuri na yanaongeza uwelewa wao na uwezo wa kutambua mambo yanayo wazunguka, wanatakiwa kuwajibika kwa sababu wao ni tabaka muhimu na nguvu kazi kubwa katika jamii”.

Akafafanua kua: “Hakika kongamano hili linafanywa kwa baraka za mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s), aliye jitolea nafsi yake kwa ajili ya ndugu yake na Imamu wake Hussein Shahidi (a.s) na kwa ajili ya Dini na ubinaadamu, naye ni kielelezo cha kuigwa katika ukarimu na kujitolea, na ndio maana kongamano hili limepewa jina lake tukufu, ili awe ndio taa linalo waongoza wasimamizi wa kongamano pamoja na washiriki”.

Akaashiria kua: “Hakika mshiriki anajukumu la kusambaza mambo aliyo fundishwa pindi anapo rudi katika mji wake au nyumbani kwake, anatakiwa afafanue mambo tata na aonyeshe haki na mengineyo, anatakiwa kufanyia kazi mambo aliyo fundhishwa kuhusu maendeleo ya binaadamu katika maisha yake ya kila siku, kwa ajili ya kutengeneza mustakbali mwema na kupata mafanikio yatakayo tufurahisha wote”.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa washiriki, ulio wasilishwa na Mustwafa Twalibu, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa wasimamizi na wahadhiri wa kongamano, akasema kua; siku hizi zilikua siku za nuru na maarifa, na tunatarajia lifanyike tena kongamano kama hili siku zingine.

Hafla ilipambwa na ngonjera iliyo fanywa na washiriki wa kongamano, na mwisho ukawa ni wakati wa kugawa zawadi na vyeti kwa washiriki wa kongamano.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni Alqamaru linalenga watu wa tabaka mbalimbali katika jamii, na kupambana na changamoto za Dini na utamaduni pamoja na za kijamii, na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo kwa kutumia elimu za kisasa bila kujenga chuki wala kuleta ugonvi na ubaguzi ambao huwa na matokea mabaya na huleta madhara makubwa katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: