Watalamu wa Alkafeel wa mafunzo ya uokozi vitani watoa kundi la thelathini la wahitimu wa mafunzo yao…

Maoni katika picha
Katika kuandaa wapiganaji na kuwafundisha namna ya kujilinda na kuokoa uhai wa wengine, na miongoni mwa semina zake endelevu, watalamu wa Alkafeel wa mafunzo ya uokozi vitani wametoa wahitimu wa kundi la thelathini walio fundishwa namna ya kumsaidia majeruhi vitani, wahitimu wa kozi hii ni wapiganaji wa Hashdi Sha’abi.

Hafla ya ufungaji wa mafunzo haya yaliyo pewa jina la (Hema la Ashura) imefanyika katika ukumbi mkuu wa jengo la Shekh Kulaini lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Juma Tatu (21 Muharam 1440h) sawa na (1 Oktoba 2018m), ilihudhuriwa na ugeni maalumu kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu na kundi kubwa la wasimamizi na wakufunzi wa wapiganaji walioshiriki katika mafunzo haya na mafunzo yaliyo tolewa siku za nyuma.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukafuata ujumbe wa wakufunzi ulio wasilishwa na mganga mkuu Dokta Osama Abdulhassan, ambaye alibainisha kua: “Sababu zilizo pelekea kuanzishwa kundi la Watalamu wa Alkafeel na kuendelea kutoa mafunzo, hakika watalamu wa Alkafeel ni mbegu iliyo toka ndani ya Atabatu Abbasiyya baada ya kuonekana haja kubwa ya kuanzishwa kundi hili, kwa ajili ya kuokoa majeruhi wanao patikana vitani wakati wa vita kali waliyo pigana majemedari wa Iraq dhidi ya magaidi”.

Akafafanua kua: “Hakika watu waliohitimu mafunzo yetu walifanikiwa kuokoa mamia ya majeruhi, wale walio hitimu katika mafunzo tuliyo toa siku za nyuma, bado tunaendelea kutoa mafunzo haya kwa wapiganaji wa vikosi mbalimbali”.

Akaongeza kua: “Hakika haya ni mafunzo ya kundi ya thelathini mfululizo, na washiriki walikua (18) kutoka katika kikosi cha Ali Akbar na harakati ya Nujabaa pamoja na baadhi ya madaktari kutoka hospitali ya Hashimiyya iliyopo katika mji wa Baabil, kwa kuwa siku hizi tupo katika msimu wa Ashura, mafunzo haya tumeyapa jina la (Hema la Ashura), washiriki wamefundishwa mbinu mbalimbali za kumuokoa na kuondoa majeruhi katikati ya vita, na yalidumu kwa muda wa siku saba”.

Mwishoni mwa ujumbe wake Dokta Osama Abdulhassan, alitoa wito kwa vikosi vyote vya wapiganaji waje kujiunga na mafunzo haya na akasisitiza umuhimu wake, akasema kuwa mafunzo wanayo toa yanaviwango vya juu kabisa sawa na mafunzo yanayo tolewa na watalamu wa Ulaya”.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa kutoa shukrani kutoka kwa washiriki wa mafunzo hayo, ulio wasilishwa na Sajjaad Hussein kwa niaba ya wenzake, alianza kwa kuishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kisha akawashukuru wataalamu wa Alkafeel kwa kutoa mafunzo muhimu kama haya, ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuokoa mamia ya majeruhi na kupunguza hasara katika safu ya wapiganaji, akaelezea faida kubwa waliyo pata katika mafunzo haya.

Mwisho kabisa washiriki wa mafunzo wakapewa vyeti vya kuhitimu, vyeti hivyo vinakubalika kimataifa hata katika nchi za Ulaya, pia hafla ilishuhudia maonyesho ya sehemu ya mafunzo waliyo pewa, yaliyo onyesha wazi ujuzi walio pata uano wawezesha kumsaidia majeruhi katika uwanja wa vita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: