Kufuatia kumbukumbu ya kushambuliwa kubba tukufu la Maimamu wawili Askariyani: Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yafanya maonyesho ya Skaut ya awamu ya tatu…

Maoni katika picha
Kufuatia tukio linalo huzunisha la kuvunjwa kubba la Maimamu wawili Askariyaini (a.s) katika mji wa Samara na maadui wa ubinaadamu, Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya jioni ya Alkhamisi (23 Muharam 1440h) sawa na (4 Oktoba 2018m) wamefanya maonyesho katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wameyapa jina la (Maonyesho ya Skaut Alkafeel) haya ni maonyesho ya tatu katika program ya (Labbaika yaa Hussein), yamehudhuriwa na viongozi wa Dini, wakisiasa na kijamii.

Rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Leeth Mussawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Hii ni kazi nzuri inayo fanywa na ndugu zetu wa idara ya watoto na makuzi hususan ofisi ya hema za Skaut imekua ikifanya mambo mazuri kijamii, yanayo lenga kujenga mazingira bora kwa wanachama wa hema za Skaut”.

Akaongeza kua: “Leo tumeshuhudia maonyesho haya ya kazi za mikono zilizo fanywa na baadhi ya wanachama wa Skaut, kupitia picha hizi tumeona ukubwa wa fikra zilizo tumika katika kufanya kazi hii, na baadhi ya picha zinatukumbusha mazingira waliyoishi raia wa Iraq wakati wa mapigano makali na magaidi ya Daesh”.

Akafafanua kua: “Baadhi ya fikra zilizo wasilishwa (kupitia picha) zinaonyesha kiwango cha juu cha imani ya vijana na uwelewa, pia zinaonyesha uwiyano baina ya nguvu na elimu na namna ya kufaidika na athari za utamaduni katika kutengeneza nguvu ya kweli”.

Katika mazungumzo mengine tuliyo fanya na kiongozi wa kitengo cha hema za Skaut Ustadh Ali Hussein Abdu-Zaid alisema, “Maonyesho yatafanyika siku tatu, kuanzia siku ya Alkhamisi hadi siku ya Juma Mosi (06/10/2018m), zitaonyeshwa karibu kazi (70) za mikono, za aina mbalimbali kama vile:

  • 1- Picha za mji wa Samara, kuanzia hatua ya kubomolewa hadi hatua ya ujenzi na zinazo onyesha hatua ya mwisho kabisa katika ujenzi.
  • 2- Picha zinazo husu fatwa tukufu ya kujilinda, pamoja na ushindi walio pata wapiganaji wa Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh.
  • 3- Mabango yanayo onyesha harakati za Skaut (yanaonyesha kazi za kiufundi zinazo fanywa na baadhi ya wanaskaut) na nyingi ya kazi hizo zinahusu tukio la Husseiniyya.
  • 4- Kazi za mikono zinazo onyesha nafasi ya Marjaa Dini mkuu katika miaka yote iliyopita, mambo ambayo ulimu hauwezi kuyaelezea, hadi mwisho wake ukawa ni kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda.
  • 5- Mabango yanayo onyesha vita ya nafsi na changamoto inazo pata jamii kutokana na vyombo vya habari, pamoja na picha zinazo onyesha harakati mbalimbali za Jumuiya na kazi inazofanya.
  • 6- Maonyesho madogo ya Skaut, yanayo onyesha kinacho fanyika katika hema zake, pamoja na hema la matangazo litakalo tumika kuonyesha baadhi ya filamu na baadhi ya ripoti maalumu kuhusu jumuiya ya Skaut”.

Akaongeza kua: “Hakika kila kinacho onyeshwa katika maonyesho haya, kinatokana na kipaji cha mwanaskaut kilicho julikana wakati wa mazowezi ya Skaut, vipaji hivyo vimeonyeshwa wazi kupitia picha na mabango haya”.

Akafafanua kua: “Lengo la maonyesho haya ni kukumbusha unyama uliofanywa wa kuvunja kubba la Maimamu wawili Askariyaini (a.s) ili jambo hilo lisisahaulike, pamoja na kuonyesha harakati za Husseiniyya kwa walimwengu na baadhi ya mambo muhimu kwa mazuwaru kupitia maonyesho”.

Kumbuka kua Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ambayo ipo chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya shughuli mbalimbali zinazo saidia kwa kiasi kikubwa kuandaa kizazi kinacho fuata misingi mitukufu ya uislamu inayo tokana na mwenendo sahihi wa Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: