Kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chatoa maelekezo kuhusu ziara ya Arubaini ya mwaka huu (1440h / 2018m)…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu jioni ya Juma Mosi (26 Muharam 1440h) sawa na (6 Oktoba 2018m) kimetoa maelekezo kwa wenye mawakibu zitakazo shiriki katika maombolezo ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na kuwaomba wayazingatie na kuyafuata, maelekezo hayo ni:

  • 1- Wahudumu wote wa mawakibu wazingatie kuswali kwa wakati, kila mtu aswalie katika maukibu yake, haitakiwi kufungua vipaza sauti wakati wa swala pia wanatakiwa kuzingatia ukubwa wa sauti, vipaza sauti vyote vinatakiwa kufungwa saa sita usiku.
  • 2- Wahudumu wote wa mawakibu Husseiniyya wanatakiwa kulinda heshima ya mji mtukufu wa Karbala.
  • 3- Mawakibu zote za Husseiniyya zinatakiwa kuingia kwa kufuata ratiba kutokana na aina ya maukibu, kama ni ya Zanjiil au matam, mawakibu za zanjiil ziatatakiwa kuingia siku ya (16 na 17 Safar) na mawakibu za matam siku ya (18 na 19 Safar).
  • 4- Hairuhusiwi kuweka maukibu katika sehemu za bustani za umma na katikati ya barabara, na inatakiwa kutunza miti ya barabarani (inayo pamba mji wa Imamu Hussein –a.s-).
  • 5- Mawakibu zinatakiwa kuingilia mlango wa kibla ya Imamu Hussein (a.s) na kutokea mlango wa Qaadhi Hajaat na kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, kisha zinaingia katika Atabatu Abbasiyya tukufu halafu zinaondoka na kurudi katika eneo lao.
  • 6- Tunapenda kuzijulisha mawakibu Husseiniyya zote, hakutakua na ruhusa ya kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya viwanja vya haram mbili Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuepusha msongamano.
  • 7- Kiongozi wa maukibu anatakiwa aonyeshe kibali alicho pewa na polisi wa mkoa wa Karbala pamoja na kitambulisho alicho pewa na kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu / Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 8- Kiongozi wa maukibu anawajibika kulinda usalama wa watu wake, na anatakiwa azuwie kuingia watu asio wajua katika maukibu yake, vile vile anatakiwa atangulize watu wanao julikana watakao watambulisha watu wa maukibu yake wakati wa kuingia katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
  • 9- Vipaza sauti na kamera vitakaguliwa na watu wa usalama.
  • 10- Hairuhusiwi kubeba siraha au vitu vyenye ncha kali pamoja na vifaa vya kunyunyiza maji.
  • 11- Hairuhusiwi kubeba picha ya kiongozi yeyote wa Dini, ili kuhakikisha kila kinacho fanyika ni kwa ajiliya Imamu Hussein (a.s).
  • 12- Hairuhusiwi maukibu inayo fanya Tatbiir (kujitoa damu) katika ziara ya Arubaini, kwa sababu Tatbiir hufanywa (na baadhi ya watu) siku ya mwezi kumi Muharam peke yake (siku ya damu) kutokana na mazingira ya siku hiyo, yeyote atakaye fanya Tatbiir katika ziara hii uongozi wa Alkafeel utamchukulia nidhamu za kisheria.
  • 13- Hairuhusiwi kufanya maigizo yasiyo endana na tukio la Arbaini, maigizo yanayo kubaliwa ni yale yanayo endana na tukio halisi na yafanyiye katika sehemu ya maukibu, ifahamike kua wakati mateka na Imamu Sajjaad (a.s) wanarudi hawakushindikizwa na majeshi wala hawakufungwa minyororo.
  • 14- Hairuhusiwi kunyanyua fimbo, bendera au bango lisilo endana na ziara ya Arubaini.
  • 15- Maukibu zitapewa vitabu maalumu na mkuu wa kamati ya mahusiano ya mawakibu Husseiniyya aliye idhinishwa na uongozi wa polisi wa mkoa mtukufu wa Karbala katika geti za kutoka na kuingia kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao.
  • 16- Kuthibitisha sehemu zitakazo kuwepo mawakibu ndani na nje ya mji ni miongoni mwa majukumu ya kiongozi wa idara ya mawakibu.
  • 17- Kuheshimu maelekezo na mwongozo wa kuingia kwa mawakibu yaliyo tolewa na kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya / Atabatu Abbasiyya tukufu, na kutoa ushirikiano kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu pamoja na watumishi wa mawakibu Husseiniyya na wafanyakazi wa idara za usalama.
  • 18- Hairuhusiwi kubeba vichwa na mizoga katika maigizo hata ndani ya hema la maukibu, kwani kufanya hivyo ni kuwadhalilisha wahusika na hakuendani na tukio lenyewo.
  • 19- Mawakibu zitaingia mwezi (15 na 16 Safar) peke yao.
  • 20- Kila maukibu inatakiwa iwe na kifaa cha zima moto na kiwekwe sehemu ya wazi kwa ajili ya kupambana na hatari yeyote ya moto kama ikitokea –Allah atuepushie-.
  • 21- Kutunza barabara na mali za umma, ikiwa ni pamoja na njia za maji, hairuhusiwi kufunga hema au kujenga banda katika njia za maji au kutupa taka humo, bali hairuhusiwi kufanya jambo lolote litakalo kwamisha mtiririko wa maji.
  • 22- Hairuhusiwi kutumia kuni ndani ya mji, inatakiwa itumike gesi peke yake.
  • 23- Hairuhusiwi kuchanganyika na wanawake katika maukibu ya Zanjiil na matam.
  • 24- Inatakiwa kuweka bango la utambulisho katika mlango wa maukibu, litakalo kua na jina la maukibu pamoja na jina la kiongozi wa maukibu na namba zake za simu.
  • 25- Inaruhusiwa maukibu moja kuingia mara mbili, mara moja ya Zanjiil na nyingine ya Matam, kiongozi anatapewa ukomo wa idadi za kuingia.
  • 26- Likitokea tatizo lolote karibu na maukibu yako toe taarifa katika kituo cha ulinzi kilicho karibu yako.
  • 27- Watumishi wote wa mawakibu wanatakiwa kuondoa vifaa vyao vyote mara tu baada ya kumalizika msimu wa ziara.
  • 28- Hairuhusiwi kujitoa damu wala kupiga ngoma ndani ya Ataba tukufu, wala haturuhusu kuingia na mikokoteni mikubwa inayo beba spika, ukubwa wa mkokoteni usizidi (mt 1 upana na 1.5 urefu).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zenu wote na awaruzuku mwisho mwema na shifaa ya Hussein (a.s) siku ya kiyama hakika yeye ni mwingi wa kusikia na mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: