Shirika la uchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limesaini mkataba pamoja na shirika la Karbala kwa ajili ya kuingiza wanyama na kuku katika machinjio ya Karbala yaliyopo barabara ya (Karbala – Baabil) kwenye kitongoji cha Ibrahimiyya, kwa ajili ya uzalishaji wa nyama.
Hatua hii imefikiwa chini ya baraka za kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuongeza pato la taifa na kuingiza nyama za kuku katika soko la Iraq, sambamba na kutoa kazi kwa watu wengi wenye uwezo wa kufanya kazi, fahamu kua machinjio hii itafanya kazi kisasa zaidi na inavifaa rafiki kwa mazingira.
Tunapenda kusema kua; shirika la uchumi Alkafeel ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, linaendesha miradi mingi ya kiuchumi ambayo inamchango mkubwa katika kuendeleza viwanda na kilimo na linachangia soko la taifa kwa kuingiza bidhaa zinazo tengenezwa nchini na kushajihisha uzalishaji wa taifa.