Kwa yeyote anaye taka kushiriki katika shindano hilo aangalie masharti ya ushiriki na atume filamu yake kwa kufuata masharti hayo, ambayo ni:
- 1- Filamu izungumzie matukio ya Imamu Hussein na athari yake (pia iendane na malengo ya kongamano).
- 2- Filamu izingatie utukufu wa Imamu Hussein na ifuate sheria na kanuni za dini na jamii pamoja na adabu za kiislamu.
- 3- Filamu iwe haijawahi kuonyeshwa mahapa popote (katika luninga (televishen) au kwenye intanet).
- 4- Filamu isiyo kua ya lugha ya kiarabu itafsiriwe kwa kiarabu sahihi, imma kwa maandishi au kuingiza sauti.
- 5- Filamu isizidi dakika (15).
- 6- Mwisho wa kupokea filamu ni mwezi wa Rajabu 1440h.
- 7- Filamu isiwe na nembo yeyote ya mtengenezaji.
- 8- Filamu isionyeshe kufutwa au kubadilishwa na yeyote, pia inaweza kukubaliwa au kukataliwa.
- 9- Filamu itapokelewa ikiwa kwenye (dvd) na itumwe kwenye kamati ya filamu moja kwa moja au kupitia email (rabee@alkafeelnet).
- 10- Kava la (dvd) liandikwe: (Mada ya filamu, muda, jina la muandaaji, lugha iliyo tumika na jina la nchi).
- 11- Filamu zitakazo kubaliwa kushiriki katika shindano zitatangazwa na kamati kuu mwezi (20 Rajabu 1440h).
- 12- Kamati inayo simamia kongamano inahaki ya kutunza filamu hizo na kuzitumia, pia inahaki ya kuzirudufu chini ya anuani isemayo (maktaba ya filamu za Husseiniyya).
Zawadi za washindi wa shindano:
- 1- Mshindi wa kwanza: (5,000,000) milioni tano dinari za Iraq.
- 2- Mshindi wa pili: (3,000,000) milioni tatu dinari za Iraq.
- 3- Mshindi wa tatu: (2,000,000) milioni mbili dinari za Iraq.
Kuna zawadi saba zingine ambazo ni midani maalumu ya washiriki wa shindano hilo.