Ilipo fika saa nne asubuhi kwa muda wa New York Marekani kongamano la (Kurudisha nafasi muhimu na kuimarisha jamii adilifu na usalama enevu) linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa kushirikiana na taasisi ya Imamu Khui na umoja wa kielimu na turathi limeanza.
Kongamano hilo linafanyika katika ukumbi wa uchumi ndani ya jengo la umoja wa mataifa katika mji wa New York likiwa na washiriki wengi ambao ni viongozi wa kiislamu na wasio kua waislamu kutoka nchi tofauti, katika kongamano hili jumla ya mada tatu zitawasilishwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na mada mbili zitawasilishwa na Atabatu Abbasiyya. Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika kongamano hili unatokana na nafasi yake ya ubaba kwa waislamu wote, hasa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wa milengo na mitazamo yote.
Kumbuka kua kongamano hili linafanyika ndani ya jengo la makao makuu ya umoja wa mataifa huko New York Marekani kuanzia tarehe nane mwezi huu wa kumi, na kuhudhuriwa na viongozi wa dini tofauti na wasomi mbalimbali, pamoja na waandishi wengi wa habari kwa ajili ya kurusha tukio hili muhimu.
Tutakujuzeni zaidi kadri tutakavyo endelea kupata taarifa…