Imeanza kutekelezwa ratiba ya kongamano la (Elimu za kiismalu baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Kotagen: katika kuhudumia sekta ya elimu na jamii), linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kotagen cha Ujerumani.
Kongamano hili linafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa chuo kikuu, na limehudhuriwa na viongozi wengi wa kisekula pamoja na balozi mdogo wa Iraq iliyopo Ujerubani.
Rais wa ugeni unao shiriki katika kongamano hili Ustadh Jawaad Hasanawi amebainisha kua:
Kutokana na mtazamo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kusambaza fikra na utamaduni wa kiislamu, pia kutokana na agizo la kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi. Mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa Ulaya kwa kushirikiana na ofisi ya katibu mkuu, wameandaa kongamano la kielimu na kitamaduni pamoja na chuo kikuu cha Kotagen chini ya anuani isemayo: (Elimu za kiislamu baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Kotagen: katika kuhudumia sekta ya elimu na jamii), lengo la kongamano hili ni kujadili mambo yanayo unganisha umma, mataifa na dini tofauti na kufanya mazungumzo ya kujenga maelewano kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa kuishi kwa amani baina ya mataifa na umma tofauti chini ya mafundisho ya dini tofauti zinazo tokana na Mwenyezi Mungu mtukufu ambaye ndiye aliye leta Uislamu na dini zingine kwa ajili ya kuweka amani na rehema kwa walimwengu.
Akaongeza kua: Hakika hili ndio lengo la kila mtu mwenye akili, kuhakikisha walimwengu wanaishi kwa amani na usalama, hasa katika zama hizi ambazo tunasikia sauti kila sehemu ya dunia inayo himiza na kufanya uvunjifu wa amani na uharibifu mkubwa kila mahala.
Akasema: Napenda kufahamisha kua chuo kikuu cha Kotagen ambacho kina kitengo maalum cha masomo ya kiislamu kimeshirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuendesha kongamano hili na wameandaa mada na kuziwasilisha kwa kutumia maneno ya kiarabu, wamewatumia watumishi wao wanaojua kiarabu au wenye asili ya kiarabu, jambo hili limepewa umuhimu mkubwa na kamati inayo simamia kongamano tuna muomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawezeshe na awape mafanikio.
Naye Dokta Ahmadi Juma ambaye ni balozi mdogo wa Iraq katika mji wa Frankford amesema kua: Hili ni kongamano la kwanza kufanyika katika nchi za Ulaya chini ya chuo kikuu kikubwa cha Ujerumani, chuo cha Kotagen kinacho fundisha masomo ya uislamu, hivyo kongamano hili ni fursa nzuri ya kubadilishana mawazo wageni waliokuja hapa Ujerumani wakiwa na mada tofauti, kama vile; elimu na jamii, elimu za kiislamu na namna ya kujenga amani, pia kuna maonyesho ya kimataifa yanayo fanyika katika mji wa Frankford ambayo Atabatu Abbasiyya inashiriki, nayo ni miongoni mwa maonyesho makubwa katika bara la ulaya, sambamba na nadwa zinazo fanyika ikiwa ni pamoja na nadwa ya Balin.
Akaongeza kua: Hii ni fursa kubwa na muhimu inayo saidia kuzileta pamoja fikra za wairaq na wajerumani kupitia kongamano hili tukufu la (Wiki ya Abulfadhil Abbasi –a.s-) chini ya Atabatu Abbasiyya na chuo kikuu cha Kotagen tunawaombea mafanikio mema.
Akamaliza kwa kusema: Jambo hili ni zuri na muhimu sana kuona Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya harakati za kimataifa, sio katika ulimwengu wa kiislamu peke yake lakini pamoja na dini zingine vilevile na katika nchi zingine, hasa nchi ya Ujerumani ambayo inaonyesha umuhimu wa kushirikiana na nchi za mashariki ya kati.
Mwishoni mwa siku ya kwanza zikagawiwa zawadi za midani iliyo andikwa jina la Abulfadhil Abbasi (a.s) kama ishara ya kuonyesha kujali kazi nzuri iliyo fanyika.