Mwezi wa Safar

Maoni katika picha
Wakati umekaribia ambao watu makundi kwa makundi humiminika katika mji wa Karbala wakiwa na huzuni kubwa huku wanatokwa machozi wakikumbuka tukio la watu ambao walihuzunikuiwa mbinguni kabla ya duniani.

Hizi hapa mawakibu za kutoa huduma zimeenea katikati na kusini mwa Iraq, zimeanza kufunga hema zake kwa ajili ya kujiandaa kutoa huduma kwa mamilioni ya watu watakao kuja kutoka kila kona ya dunia kwa ajili ya kumzuru bwana wa mashahidi na ndugu yake (a.s).

Katika mwezi wa Safari hakuna anuani zaidi ya Hussein, wala hakuna bendera inayo pepea juu ya bendera yake, wala hakuna sauti inayo sikika zaidi ya jina lake, wala machozi yanayo toka ispokua kwa sababu ya kilio chake, na watu hujipiga vifua kwa ajili ya msiba wake, katika mwezi wa Safar ukarim huwa mkubwa sana, unapo tajwa ukarimu wa raia wa Iraq hutajwa pamoja na Hussein (a.s), hatujui tuseme raia wa Iraq ndio wakarim au wewe Hussein ndio mkarim.

Katika mwezi wa Safar mataifa mbalimbali hukutana na watu wa tabaka mbalimbali kila mmoja anamuhudumia mwenzake kwa jina la Hussein, katika mwezi wa Safar hakuna tofauti ya muarabu na asiye kua muarabu, utaifa wote huondoshwa mbele ya Hussein (a.s), katika mwezi wa Safar kila mmoja huwa yupo katika amani, Mwenyezi Mungu amejaalia mapenzi katika nyoyo za watu wanaokwenda katika ardhi ya Tufuuf (Karbala).

Katika mwezi wa Safar hutajwa sana jina la Hauraa Zainabu (a.s) balozi wa Twafu na kamanda wa Karbala na ulimi wa mapinduzi ya Husseiniyya, katika mwezi wa Safar nyoyo za waumini huungana katika kupandisha bendera moja isiyo kua na mshindani ambayo ni bendera ya (Labbaika yaa Hussein)…

Kwa ufupi, katika mwezi wa Safar huwa kila ardhi ni Karbala na kila siku ni Ashura.

Watu wa Karbala kama kawaida yao hufungua milango kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru, huwakaribisha katika nyumba zao, mazuwaru hua kama ndio wenye nyumba na wenye nyumba kama ndio wageni, huhesabu mchana na usiku kwa shauku ya kufika siku hizo, huwakilisha utumishi wa Abulfadhil Abbasi kwa Hussein (a.s), katika mwezi wa Safar kila nyumba ya Karbala ni maukibu na kila mtu ni mtumishi, watoto kwa wakubwa wanawake kwa wanaume.

Katika mwezi wa Safar mandhari ya ulimwengu wa kiislamu hujaa mapenzi, ziara ya Arubaini ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu haifanani na haitafanana na kumbukumbu yeyote katika historia.

Katika mwezi wa Safar Iraq humkaribisha kila mtu na Karbala huwahifadhi watu wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: