Picha za Ataba tukufu za Iraq zateka jengo la umoja wa mataifa New York.

Maoni katika picha
Pembezoni mwa kongamano la kimataifa linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika jengo la umoja wa mataifa kwa kushirikiana na taasisi ya Imamu Khui na umoja wa tafiti za kielimu na turathi wa New York, yameratibiwa maonyesho ya picha yaliyo pewa jina la: (Mahdi Shahada), picha za kuonyeshwa zilichaguliwa Iraq na kamati maalumu ya watalamu wa mambo ya picha.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na msimamizi mkuu wa maonyesho haya Ustadh Samir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kupitia ushiriki wetu katika kongamano hili, tulikusudia kutumia kila njia itakayo tuwezesha kufikisha ujumbe wa Ataba tukufu za Iraq ikiwa ni pamoja na kutumia njia ya picha, maonyesho haya ya picha ni sawa na sawa na kupeleka akili za mtazamaji katika Ataba tukufu za Iraq, zinaonyesha moja kwa moja namna watu wa aina mbalimbali mamilioni ya waumini wanavyo miminika katika Ataba hizo kufanya ziara kila mwaka”.

Akabainisha: “Hakika picha hizo pia zinaonyesha uharibifu uliofanywa na magaidi wa Daesh Iraq kwa kuvunja maeneo matukufu na turathi za taifa, na ushujaa wa pekee walio onyesha raia wa Iraq walio simama imara dhidi ya Daesh na kuwaangamiza na hivi sasa wanajenga taifa lao”.

Akafafanua kua: “Katika maonyesho haya tumegawa picha katika sehemu zifuatazo:

  • 1- Picha za Ataba mbili za Karbala na pembezoni mwake, zinazo onyesha hatua za ujenzi wa Ataba hizo ulio fanyika zamani na unaofanyika hivi sasa.
  • 2- Picha za mazuwaru wanaokuja katika Ataba tukufu za Iraq kutoka kila sehemu ya Dunia na huduma wanazo pewa njiani.
  • 3- Picha za misaada ya kibinaadamu iliyo kua inatolewa na askari wa Iraq wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh ya kukomboa maeneo yaliyo tekwa, pamoja na namna walivyo saidia familia za wakimbizi.
  • 4- Picha za uharibifu ulio fanyika katika Atabatu Askariyya huko Samara baada ya shambulizi la mwaka (2006 na 2007m) pamoja na picha za kurudia kuijenga upya.

Kumbuka kua picha zinazo onyeshwa hapa zilichaguliwa katika hazina ya Atabatu Abbasiyya tukufu nchini Iraq na zikachapishwa New York, kila picha imewekewa maelezo yake, maonyesho haya yamepata mwitikio mkubwa sana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: