Miongoni mwa program za wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho ya kimataifa yanayo fanyika Frankford wakiwa na zaidi ya aina 175 za vitabu, ushiriki huu unachukuliwa kua wa kwanza wa aina hii kwa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo shiriki katika maonyesho haya yamebeba aina mbalimbali za machapisho ya Ataba tukufu yanayo husu sekta tofauti na yaliyo chapishwa katika ubora mkubwa.
Vitengo na vituo vya kitafiti vinavyo shiriki katika maonyesho haya ni: Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, kitengo cha habari na utamaduni, kituo cha kimataifa Al-Ameed cha utafiti na masomo, kituo cha masomo ya kimkakati na kituo cha kuhuisha turathi ambacho kipo chini ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kumbuka kua haya ni miongoni mwa maonyesho makubwa kimataifa, kuna zaidi ya taasisi na vitengo vya usambazaji 7000 vinavyo shiriki katika maonyesho haya, na yatafanyika kwa muda wa siku tano mfululizo, kuanzia tarehe 10/10/2018m hadi 14/10/2018m.