Ujumbe wa Atabatu Abbasiyya katika ugeni wa maktaba ya chuo kikuu cha Kotagen Ujurumani…

Maoni katika picha
Miongoni mwa program za wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zilizo anza tarehe nane mwezi huu wa kumi zenye vipengele mbalimbali na zinazo fanyika katika miji mitatu tofauti ya Ujerumani, ambayo ni: Kotagen, Balin na Frankford, ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea maktaba ya chuo kikuu cha Kotagen kuangalia hazina iliyopo katika maktaba na uduma zinazo tolewa na maktaba hiyo kwa wasomaji wake, sambamba na kuangalia vifaa kazi walivyo navyo na nakala kale za kiababu zilizopo ndani ya maktaba hiyo kubwa.

Ziara hii ipo ndani ya ratiba ya shughuli za wiki ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inayo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kotagen cha Ujerumani, lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi za Ujerumani, sambamba na kuzitambulisha taasisi hizo mambo yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ikiwa ni pamoja na huduma inazo toa kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Baada ya kutembelea maktaba hiyo, Atabatu Abbasiyya tukufu iliwapa baadhi ya machapisho yake, kama vile kitabu cha Alammah Ordibadi pamoja na majarida ya kielimu.

Tunapenda kukumbusha kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha program ya wiki ya kitamaduni nchini Ujerumani waliyo ipa jina la (wiki ya Abulfadhil Abbasi –a.s-) katika miji mitatu ya Ujerumani ambayo ni: Kotagen, Balin na Frankford, pamoja na nadwa inayo elezea mambo yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na huduma inazo toa kwa mazuwaru na makundi ya jamii za wairaq, sambamba na kuonyesha miradi yake mikubwa katika sekta ya ujenzi na elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: