Taasisi ya Imamu Khui huko New York yaupa zawadi ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu na yasifu uratibu mzuri wa kongamano…

Maoni katika picha
Taasisi ya Imamu Khui iliyopo New York umewazawadia wageni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu waliokuja kushiriki katika kongamano la kimataifa lililofanyika kwa mara ya kwanza katika jengo la umoja wa mataifa kwa ushirikiano wa taasisi hiyo na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na umoja wa tafiti za kielimu na turathi, lililo pewa jina la: (Kurudisha heshima ya elimu kwa ajili ya kuupa nguvu uadilifu wa kijamii), kutokana na kazi walizo fanya wakati wa kongamano pamoja na wakati wa maandalizi ya kongamano yaliyo chukua zaidi ya miezi mitano, pia kutokana na upekee wa mada waliyo wasilisha katika kongamano iliyo kua inahusu famasia, bila kusahau kazi kubwa iliyo fanywa na wageni hao ya kuratibu na kusimamia kongamano hilo.

Shughuli ya kukabidhi zawadi imefanyika ndani ya makao makuu ya taasisi hiyo na kuhudhuriwa na rais wa taasisi Shekh Fadhili Sahlani pamoja na jopo la watumishi wake.

Katika ujumbe alio toa Shekh Sahlani, ameshukuru sana na kasifu kazi nzuri iliyo fanywa na wageni waliokuja kushiriki katika kongamano hilo, akabainisha kua: “Hakika walikua msaada mkubwa kwetu, kutokana na msaada wao tumeweza kufanya tukio kubwa la kimataifa kwa mara ya kwanza ndani ya jengo la umoja wa mataifa, tukio hili maandalizi yake hayakua ya muda mfupi, tulifanya vikao mara kadhaa na tukaweka mpango kazi na kuchagua mada zinazo endana na mazingira ya sasa, tuliweka pamoja fikra zetu na tukaweza kutoka na jambo zuri, huu ni ushahidi wa mshikamano mzuri na wenye manufaa makubwa katika uislamu na mazingira tunayo ishi, hakika kongamano lilipangiliwa vizuri na limekidhi vigezo vya kimataifa, tunatarajia jambo hili lifanyike tena katika matukio mengine yajayo, zawadi tunayo ikabidhi kwa watu hawa watukufu ni ndogo sana”.

Rais wa ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Riyadhi Amidi “Aliishukuru sana taasisi hiyo ambayo imetumia uwezo wake wote kwa ajili ya kuratibu na kuhakikisha kongamano hili linafanyika, na kuishirikisha Atabatu Abbasiyya kwa mara ya kwanza, kwa namna ya pekee kabisa kongamano hili kutokana na rehma ya Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) limekua na mafanikio makubwa katika mambo yote yaliyo fanyika ndani ya ratiba hata yale ya pembeni ya ratiba”.

Kumbuka kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano hili unatokana na nafasi yake ya ubaba kwa waislamu wote, hasa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), nayo ni sehemu ambayo nyoyo za watu wote wa Dini tofauti hutamani kufika mahala hapo, Ataba hiyo ni shule ya ushujaa, kujitolea, uaminifu na undugu, shule ambayo umefundisha Dunia vizazi na vizazi namna ya kujitolea kwa ajili ya kulinda haki na kuondoa batili.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi zake za kitamaduni na kielimu, zinafanya kazi kwa mlengo wa kati, ili ziweze kuzuwia mashambulizi ya kifikra yanayo elekezwa katika umma wa kiislamu, na kutatua matatizo ya upotoshaji katika jamii ya kiislamu, zimefanya kazi kubwa kwa ajili ya jambo hilo, zimesha fanya makongamano mengi ndani na nje ya Iraq, na zinaendelea na mwenendo huo katika jamii za raia wa Iraq na duniani kote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: