Miongoni mwa maandalizi ya ziara ya Arubaini: Kitengo cha angalizi wa kihandisi chatengeneza daraja la chuma la muda kwa ajili ya mazuwaru…

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wamekamilisha kazi ya kutengeneza daraja la chuma la muda kwa ajili ya kutumiwa na mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Daraja hili hutengenezwa kila mwaka mapema kabla ya msongamano wa mazuwaru wanaokuja Karbala kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini, hujengwa daraja la juma kwa ajili ya kupunguza msongamano wa mazuwaru na kupunguza mwingiliano wa matembezi ya mawakibu na watu wa kawaida wakati wa kutoka katika haram tukufu ya Abbasi upande wa kusini magharibi katika mlango wa Imamu Hassan na Imamu Hussein (a.s).

Daraja hilo limeundwa kutokana na vipande vya vyuma vilivyo onganishwa kiutaalamu, lina upana wa mita (8) na lina sehemu mbili ya waendao na warudio, kila sehemu inaupana wa mita (4) na urefu wa kwenda juu ni zaidi ya mita (4), pia linavipande vya mbao ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita (2.40) na upana wa mita (1.22) vilivyo wekwa pembeni ya daraja kwa ajili ya kulinda usalama wa wapitaji.

Tunapenda kufahamisha kua kitengo cha uangalizi wa kihandisi ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinacho fanya kazi za aina mbalimbali kila siku na kina mchango mkubwa katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa upande mwingine tunaweza kusema kua Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha maandalizi yote ya lazima kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru watukufu wa ziara ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: