Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu watembelea taasisi ya Alghadiir na kituo cha Imamu Ali (a.s) katika mji wa New York na kuangalia harakati na huduma wanazo toa…

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ulioshiriki kongamano la kimataifa lililo fanyika katika jengo la umoja wa mataifa miongoni mwa malengo yao ni kutembelea taasisi na vituo vya kidini vinavyo saidia waislamu wahamiaji, kwa ajili ya kuangalia utendaji wao na changamoto zao, ziara hizo zinazipa moyo taasisi na vikundi hivyo wa kuboresha utendaji wao.

Miongoni mwa taasisi zilizo tembelewa ni taasisi ya Alghadiir, ambayo ni taasisi ya kidini na kitamaduni ipo upande wa magharibi ya jimbo la New York, ugeni huo ulipokelewa na kiongozi wa taasisi hiyo Shekh Muan Sahlani ambaye aliongea maneno mazuri sana katika mapokezi yake, kisha akaelezea kwa ufupi shughuli zinazo fanywa na taasisi hiyo ambayo imejikita katika kulea na kujenga maadili mema kwa familia za waislamu wanaohamia katika taifa hilo, sambamba na kufanya semina za Qur’ani na masomo mbalimbali yanayo endana na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), pamoja na kusambaza mafundisho ya mwenendo wao unao wakilisha tabia ya dini tukufu ya kiislamu.

Sehemu nyingine waliyo tembelea ni kituo muhimu cha Dini kilichopo katika mji wa New York, kituo cha Imamu Ali (a.s), ambacho kinahudumia waislamu wahamiaji pia, ugeni huo ulipokelewa na kiongozi wa kituo hicho Sayyid Ali Ridhawi ambaye alielezea kwa ufupi historia na harakati za kituo hicho, ambacho ni kituo maarufu zaidi, akashukuru sana kutembelewa na ugeni huo mtukufu, akasema kua; kituo hiki hakijawahi kutembelewa na ugeni wowote kutoka katika Ataba tukufu, akawapongeza kusafiri umbali mkubwa kwa ajili ya kuja kutoa picha halisi ya uislamu wa kweli.

Mjumbe wa ugeni huo Dokta Mushtaqu Abbasi Muan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kudumisha mawasiliano baina ya waislamu ni siraha kubwa sana ya kulinda utambulisho wa Dini katika mazingira yenye changamoto nyingi, sambamba na kuangalia matatizo wanayo pata wahamiaji na taasisi za Dini katika miji ya ugenini, Ataba tukufu hasa Husseiniyya na Abbasiyya zinafanya juhudi kubwa ya kujenga uhusiano na waislamu, ikiwa ni pamoja na kusaidia utendaji wa tablighi na kujenga maelewano ya kuishi kwa amani na watu wa tabaka zote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: