Katika maukibu ya pamoja: Wanafunzi wa Maahadi na Vyuo vya Iraq waomboleza msiba wa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Juma Mosi (3 Safar 1440h) sawa na (13 Agosti 2018m) yamefanyika matembezi ya pamoja ya wanafunzi wa Maahadi na Vyuo vya Iraq kwa ajili ya kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s), matembezi hayo yalianzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuelekea katika uwanja wa haram tukufu ya Abbasi, kisha wakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hadi kwa muhusika mkuu wa msiba Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwenye uwanja wa haram yake tukufu, wakati wa matembezi yao hawakuacha kuimba kaswida za kumhuzunikia mjukuu wa Mtume wetu Mtukufu (s.a.w.w).

Kuhusu maukibu hii; mwakilishi wa Atabatu Husseiniyya katika mkoa wa Nainawa Ustadh Shuaibu Ahmadi Azizi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Chuo kikuu cha Mosul kinawakilisha Iraq ndogo, kutokana na kuwa na watu wa tabaka tofauti na Dini mbalimbali kutoka katika kila kundi, leo wamekuja Karbala kutoka Mosul kwa ajili ya kumpa pole Abu Abdillahi Hussein (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Sisi wanafunzi na walimu wa chuo kikuu cha Mosul tunashiriki katika maukibu ya kuomboleza inayo jumuisha vyuo vikuu na Maahadi za Iraq ikiwa ni sehemu ya kupambana na mazingira yaliyopo pamoja na kuunga mkono umoja wa taifa la Iraq”.

Rais wa chuo kikuu cha Karbala Dokta Muniir Hamidi Sa’adi akauambia mtandao wa Alkafeel kua: “Leo vyuo vikuu vya Iraq kutoka kaskazini na kusini vimekuja kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) pamoja na waumini bora walio kufa pamoja naye”.

Akaongeza kua: “Leo hii tunanufaika moja kwa moja kutokana na mafundisho na mazingatio yanayo patikana katika tukio hili chungu, ambayo yameakisi katika maisha yetu, tunaweza kusema tukio la karibu zaidi la manufaa hayo ni ushindi ulio tokana na fatwa tukufu iliyo tangazwa chini ya kubba la Imamu Hussein (a.s), na ikawa taa lililo waangazia walio jitolea na kielelezo cha umoja na msimamo wa kupigana hadi kupatikana ushindi”.

Tunapenda kukumbusha kua mawakibu za Husseiniyya zinaendelea kumiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu mwanzo wa mwezi wa Muharam, huku watumishi wa Ataba hizo wakiwa katika maandalizi ya hali ya juu kabisa ya kuwapokea mamilioni ya mazuwaru wanaokuja katika mji mtukufu wa Karbala kwenye kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: