Idara ya nakshi na maraya yakamilisha upambaji wa kuta za ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Mafundi wa idara ya nakshi na maraya (marumaru za vioo) chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi, wamemaliza kazi ya kupamba kuta na dari la ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), umuhimu wa kazi hii unatokana na kuongeza uzuri wa mwonekano kwa kuweka rangi maalumu zinazo endana na utukufu wa eneo hili, pamoja na kubakiza mwonekano wa zamani katika maraya na kuta za ndani ya haram tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya nakshi na maraya katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi Ustadh Hassan Saidi Mahdi, ambaye amesema kua: “Kazi hii imehusisha utowaji wa maraya zilizo haribika katika kuta za ndani ya haram pamoja na kuziba sehemu za kuta zilizo pasuka kwa kutumia vitu maalumu vya ujenzi vinavyo umarisha zaidi ukuta, miongoni mwa vitu hivyo ni Graut na Sekodor, kisha ikafuata hatua ya kuskim ukuta kwa kutumia Jipsam poda kwa kiwango cha (sm 1.5), pamoja na kuweka sapoti ya vyuma katika maumbo ya nusu duara, kisha zikaendelea hatua zingine za ujenzi, ikiwa ni pamoja na kurudisha maraya za zamani ambazo hazija haribika na kubadilisha zilizo haribika kwa kuweka mpya”.

Akaendelea kusema: “Hakika kazi inayo fanywa na mafundi wa idara ya nakshi na maraya ni kubwa sana, kwani inahitaji umakini wa hali ya juu, walikua na zamu mbili (asubuhi na jioni) kila zamu ilikua na saa saba”.

Akasisitiza kua: “Kila kinacho fanywa na mafundi kuanzia usanifu, ujenzi na shughuli zote za kihandisi kinafanywa na wataalamu ambao ni raia wa Iraq, kazi imefanyika vizuri bila kikwazo chochote wala kuleta usumbufu kwa mazuwaru watukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Tunapenda kufahamisha kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na idara zake zote kinafanya kazi mbalimbali na kutekeleza miradi muhimu inayo wagusa mazuwaru moja kwa moja katika sehemu zote za Ataba na matawi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: