Taarifa iliyo tolewa na kiongozi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, Muhandisi Abbasi Mussa Ahmadi alipoongea na mtandao wa Alkafeel alisema kua: “Idara zote za kitengo cha usimamizi wa kihandisi zinafanya kazi katika sekta tofauti, zinatengeneza au kurekebisha vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu vitakavyo tumika kuwapokea na kuwahudumia mazuwaru watukufu wanaokuja Karbala kumpa pole Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini ya kifo chake pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s) na maswahaba wake.
Akaongeza kua: “Tumefanya kazi za aina nyingi miongoni mwa kazi hizo ni:
- 1- Kuongeza uwezo wa sehemu za vyoo na kuzifanya ziweze kuhudumia watu wengi zaidi kwa kuongeza matundu ya vyoo pamoja na mambo yote yanayo hitajika.
- 2- Kukarabati vyoo vya zamani na kuongeza mabomba ya maji sambamba na kukarabati njia za maji pamoja na umeme na kubadilisha milango iliyo haribika.
- 3- Kuongeza sehemu za kupumzika misafara ya watu na kuweka sehemu za wanaume na wanawake pamoja na kuzipaua, sambamba na kukarabati kumbi.
- 4- Kukarabati mafriji makubwa ya ziada kwa ajili ya kutunzia chakula na nyama kutokana na mahitaji.
- 5- Kutengeneza barabara zinazo ingia na kutoka katika sehemu hizo.
- 6- Kuongeza screen za kuelekeza mazuwaru na kuonyesha matukio mubashara kutoka ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, screen hizo zimeandaliwa kwa kushirikiana na idara ya mawasiliano ya kitengo cha miradi ya kihandisi.
- 7- Kuweka feni na viyoyozi pamoja na vitu muhimu vyote kwa ajili ya kuwawezesha mazuwaru kupumzika sehemu hizo wakati wa joto.
Tunapenda kufahamisha kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara zake mbalimbali hufanya aina nyingi sana za kazi na hutekeleza miradi muhimu ambayo kwa asilimia kubwa huwagusa moja kwa moja mazuwaru kupitia vitengo tofauti vya Ataba, fahamu kua idara za kitengo hicho zimekamilisha maandalizi yote ya kuwapokea na kuwahudumia mamilioni ya mazuwaru wanaokuja katika ziara ya Arubaini ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba zake watukufu.