Mwaka wa nne mfululizo: (Sufra) Janvi la chakula cha bibi Ruqayya latandikwa baina ya haram mbili tukufu…

Maoni katika picha
Bibi Ruqayya ana nafasi kubwa sana katika nyoyo za wapenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kutokana na matatizo aliyo pitia akiwa katika umri mdogo, alifariki baada ya kuona kichwa cha baba yake bwana wa mashahidi (a.s), kumbukumbu ya tukio hili la kuhuzunisha imefanywa jioni ya jana Juma Pili (4 Safar 1440h) sawa na (14 Agosti 2018m) kwa kutandika janvi refu zaidi la chakula linalo itwa (Janvi la chakula cha bibi Ruqayya –a.s-).

Shughuli hii imefanywa kwa mwaka wa nne mfululizo, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na Mustafa Swarraaf, baada ra Qur’ani tukufu akapanda katika mimbari mshairi bwana Muhammad Fatwimiy akasoma beti zilizo elezea kisa cha bibi Ruqayya na dhulma alizo fanyiwa na viumbe waovu zaidi, kisha akafuatia bwana Hamidi Twawirijawi na Hamidi Tamimi walio soma kaswida za kuombeleza zilizo amsha hisia za machonzi na kuwaliza watu wote walio hudhuria, shughuli hiyo ikafungwa kwa kufanya onyesho la idizo kuhusu tukio hilo lenye majonzi makubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Tunapenda kufahamisha kua janvi (sufra) inamaana ya busati la kijani lililo wekwa vipande vya miba ikiwa kama ishara ya bibi huyo alivyo tembea juu ya miba siku ya Ashura halafu kuna kandili (taa) zilizo washwa na mishumaa, kulikua na msongamano mkubwa wa waombolezaji na watu wenye shida mbalimbali hasa watoto na wanawake, pia hugawiwa chakula kwa ajili ya kuzipeleka thawabu kwake (a.s), jambo hili hufanywa na watu wa Karbala kila mwaka.

Na bendera zinaashiria wakati Ahlulbait (a.s) walipo kua Sham bibi Ruqayya alimuota baba yake Hussein (a.s) kisha akaamka kutoka usingizini na akasema: Yuko wapi baba yangu Hussein?? Mimi nimemuona katika usingizi akiwa kadhofika sana, wanawake walipo sikia hivyo wakaanza kulia na wakalia watu wote pamoja na watoto, sauti za vilio zikawa kubwa, Yazidi akaamka na akauliza: kuna habari gani?

Watumishi wake wakamuambia kilicho tokea, akawaambia wampelekee kichwa cha baba yake, wakampelekea na kumuwekea miguuni kwake, akawauliza: nani huyu? Wakamwambia: kichwa cha baba yako. Akashtuka na akapiga yowe kisha akafariki, akarejea kwa Mola wake akiwa ni mtu mtukufu na atamuambia babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu na bibi yake Zaharaa (a.s) dhulma aliyo fanyiwa.. bibi Ruqayya mtoto wa Imamu Hussein (a.s) alifia katika mji wa Kharba huko Damaska –Sham- mwezi tano Safar mwaka wa (61h) na alizikwa sehemu alipo fia. Alikufa akiwa na umri wa miaka mitatu au minne au zaidi ya hapo kidogo kutokana na tofauti za riwaya, mwandishi wa kitabu cha Ma’ali Sibtwaini ameandika kua, mtu wa kwanza aliye kufa katika (familia ya Mtume) baada ya kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) ni bibi Ruqayya aliye fia Sham.

Kaburi lake lipo umbali wa mita mia moja au zaidi kidogo kutoka katika msikiti wa Umawiyya Damaska katika mlango wa Faradis, nao ni malango mashuhuri na mkongwe zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: