Mtawa Husseini

Maoni katika picha
Mwezi kumi na tisa Muharam mwaka 61 hijiriyya, baada ya tukio chungu la Twafu, madhalimu waliupeleka msafara wa mateka ambao ni watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) wakiwa pamoja na kichwa cha bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) pamoja na vichwa vya maswahaba wake kutoka Kufa hadi Sham.. kichwa kitukufu kilionyesha karama kubwa zilizo dhihirisha kudhulumiwa kwake na usahihi wake..

Hebu tuangalie karama hizo:

Imepokewa kutoka kwa Suleiman bun Mahraan Al-A’amashi kua: Nilipokua nafanya twawafu nilimuona mtu anaomba kwa kusema: (Ewe Mola nisamehe, na mimi najua hauwezi kunisamehe!!). Akasema: nikashangazwa na hilo, nikasogea karibu yake, nikasema, ewe ndugu, upo katika haram ya Mwenyezi Mungu na haram ya mtume wake, na hizi ni siku tukufu ndani ya mwezi mtukufu, kwa nini unakata tamaa ya msamaha wake? Akasema: ewe ndugu dhambi yangu ni kubwa. Nikasema: ni kubwa kushinda mlima wa Tahama? Akasema: Ndio. Nikasema: ni sawa na milima ya Rawasi? Akasema: ndio, ukitaka nitakuambia: nikamuambia: niambie. Akasema: tutoke ndani ya haram. Tukatoka, akaniambia: mimi ni mmoja wa waliokua katika jeshi la watu waovu; jeshi la Omari bun Saadi –laana iwe juu yake- wakati wa kumuua Hussein bun Ali (a.s) na nilikua miongoni mwa watu arubaini waliobeba kichwa cha Hussein kutoka Kufa hadi kwa Yazidi, wakati tunaenda Sham tulipita katika nyumba ya Naswara, huku kichwa tukiwa tumekitungika juu ya mkuki, tulitenga chakula na tukakaa kuanza kula, ghafla tukaona mkono unaandika ukutani:

Unategemea umma uliomuuwa Hussein *** utapata shifaa ya babu yake siku ya hesabu?!!

Akasema: tukashtushwa mno na tukio hilo, baadhi yetu wakataka kwenda kuukamata ule mkono lakini ukapotea, kisha wakarudi na wakaendelea kula, ule mkono ukarudi na ukaandika kama mara ya kwanza:

Hapana, wallahi hawana muombezi *** siku ya kiyama watapata adhabu.

Watu wakasimama ili wakaukamate ukono ule ukapotea, wakakaa kuendelea kula, mkono ukarudi tena na ukaandika:

Wamemuuwa Hussein kwa hukumu ya uovu *** wamehalifu hukumu ya kitabu (Mwenyezi Mungu).

Tukaacha kula, kisha akaja mtawa, akaona nuru inawaka juu ya kichwa, akamuuliza kiongozi wetu, mnatoka wapi? Akaambiwa, tumetoka Iraq, kupigana na Hussein. Mtawa akasema: Mtoto wa Fatuma, mtoto wa mtoto wa Mtume wenu na mtoto wa ndugu wa Mtume wenu? Wakamjibu. Nido. Akawaambia: mmeangamia, wallahi kama Issa mwana wa Maryam angekua na mtoto tungembeba vichwani kwetu, lakini ninashida kwenu. Wakamuuliza shida gani? Akasema: naomba mmwambie rais wenu mimi nina dinari Elfu kumi nilizo rithi kwa wazazi wangu, naomba nimpe pesa hizo na yeye anipe kichwa hiki nikae nacho hadi mtakapo taka kuondoka nitakurudishia.

Wakamwambia Omari bun Saadi ombi la mtawa huyo, Omari akasema: chukuweni pesa hizo na mumpe kichwa akae nacho hadi tutakapo taka kuondoka ataturudishia, wakamwambia mtawa leta pesa ulizo sema tukupe hiki kichwa, mtawa akaleta mifuko miwili kila mmoja ukiwa na dinari elfu tano, Omari akazipima na kuzihesabu zikatimia, akachukua pesa na akaamuru apewe kichwa, mtawa akakichukua kichwa kitukufu, akakiosha na kukisafisha vizuri kisha akakipulizia mafuta uzuri (uturi) akakipaka miski na kafuur, kisha akakiweka miguuni kwake huku analia na kuomboleza, hadi walipo mfuata na kumuomba awarudishie kichwa hicho, akasema:

Ewe kichwa wallahi sina kitu ninacho miliki zaidi ya nafsi yangu, nakuomba itakapo fika kesho siku ya kiyama unitolee ushahidi mbele ya babu yako Muhammad ya kwamba mimi nashuhudia kua hakuna Mola ispokua Allah na hakika Muhammad ni mja wake na Mtume wake, nimesilimu mbele yako na mimi ni mfuasi wako.

Kisha akawaambia: ninahitaji kuongea na kiongozi wenu halafu ndio nimpe kichwa hiki, Omari bun Saadi akasogea karibu yake na akamwambia: nakuomba kwa jina la Mwenyezi Mungu na kwa haki ya Muhammad (s.a.w.w) usirudie kufanya mambo uliyokua unakifanyia kichwa hiki na wala usikitoe katika sanduku hili. Omari akasema: tatekeleza unayo sema. Akawapa kicha kisha akaondoka katika nyumba ile akaenda milimani kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Omari bun Saadi akaendelea na msafara wake, na akarudia kufanya yale aliyo kua akikifanyia kile kichwa, walipo karibia Damaska akawaambia watu wake: simameni. Akaomba apewe mifuko ile ya pesa, akapewa. Akaamuru ifunguliwe, ilipo funguliwa wakakuta zile pesa zimebadilika na kua kama mikaa, akaangalia sehemu za maandishi, akakuta zimeandikwa: {Wala msidhani Mwenyezi Mungu ameghafirika na wanayo fanya madhalimu} (Ibarahim: 42) na upande mwingine zimeandikwa: {Na wanao dhulumu watakuja kujua mgeuko gani watakao geuka} (Shu’araa: 227).

Akasema (Innaa lillaahi wa innaa ilaihi Raajiuuna), nimepata hasara ya Dunia na Akhera.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: