Miongoni mwa miradi inayolenga kufundisha utamaduni wa kitabu cha Mwenyezi Mungu katika nyoyo za vijana ni mradi wa Qur’ani, unao endeshwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia idara ya utafiti na masomo ya Qur’ani katika kituo cha maarifa ya Qur’ani, kuifasiri na kuichapisha, ambao ni mradi wa kiimani ulio pewa jina la (Mubalighi wa Qur’ani).
Mradi huu unalenga kuandaa mubalighaat (walinganiaji) wa kike wa uislamu asilia unao tokana na mafundisho ya kitabu (Qur’ani) na kizazi kitakatifu.
Wamechaguliwa kujiunga na mradi huu zaidi ya wanafunzi (50) kutoka katika semina za majira ya joto (kiangazi) mwaka (2018m), mradi utachukua miezi minne ambapo watafundishwa masomo mbalimbali kuhusu Qur’ani tukufu, ikiwa ni pamoja na (kuhifadhi Qur’ani tukufu, fiqhi, aqida, akhlaqi na sira) kila siku ya Juma Mosi katika wiki.
Maahadi imesha andaa walimu walio bobea katika fani za Qur’ani tukufu watakao simamia mradi huu, pamoja na kuandaa magari yatakayo waleta na kuwarudisha wanafunzi majumbani kwao kwa ajili ya kulinda usalama wao, na imeandaa kila kinacho takiwa katika mradi kwa ajili ya kuwavutia zaidi wanafunzi.