Maoni katika picha
Mazuwaru watukufu wamesisitizwa kulipa umuhimu jambo hili, kila banda linamaelfu ya vitambulifo ambavyo vimeandaliwa maalumu kwa ajili ya watoto na wazee, ambavyo vinatakiwa kujazwa jina, mkoa na namba ya simu ya mzazi, mlezi au msimamizi wake, ili iwe rahisi kwa watumishi wa vituo hivi kumpata muhusika kwa haraka na kumtambua mtu atakaye potea kwa urahisi, na kumtangaza katika vituo vyote.
Kumbuka kua mabanda ya kuongoza walio potea na walio potelewa ni miongoni mwa huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mazuwaru, katika ziara iliyo pita walifanikiwa kukutanisha maelfu ya watu waliopotea na wasimamizi wao, fahamu kua mabanda haya yanamtandao wa kielektronik ambao una fomu maalumu iliyopo katika mabanda yote, ambayo ikiingizwa taarifa za mtu aliye potea zinaonekana katika mabanda yote.