Wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) wanamiminika kutoka kusini mwa Iraq wakielekea katika mwelekea wa watu huru mji mtukufu wa Karbala kuhuisha utiifu wao kwa bwana wa mashahidi (a.s), utamkuta mdogo anamtangulia mkubwa akiwa ameshika bendera na akiwa na ari kubwa sana ya kuhuisha alama kubwa na tukufu ya Mwenyezi Mungu ambayo ni ziara ya Arubaini, ambayo huzingatiwa kua miongoni mwa alama za waumini kama ilivyo pokewa katika hadithi za Ahlulbait (a.s).
Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Safar wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) kutoka katika miji ya kusini mwa Iraq pamoja na mazingira magumu ya hali ya hewa hayaja wazuia kutembea katika njia wanayo amini kua ni njia ya pepo ya kuelekea Karbala, wanatembea huku wanahesabu saa na dakika za kukutana na kipenzi wao na Imamu wao mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), wamejaa katika njia zote zinazo elekea Karbala, huku wakiwa na shauku kubwa ya kufika Karbala, bendera zao ni za aina moja, lengo lao moja, Mwenyezi Mungu ameweka mapenzi katika nyoyo zao.
Katika picha nyingine miongoni mwa namna ya kuonyesha mapenzi kwa Imamu Hussein (a.s), mawakibu za kutoa huduma zilifunga mahema mapema na leo hii zinaendelea na kazi ya kuhudumia mazuwaru watukufu, zinatoa vyakula, vinywaji na malazi, bila kusahau nyumba za wakazi wa miji ambayo mazuwaru wanapiza ambazo ziko wazi kwa ajili ya kutoa huduma za kila aina kwa mazuwaru wanao kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s).
Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel inakuletea baadhi ya picha za matembezi hayo.