Maukibu ya kuomboleza ya pamoja: watumishi wa Ataba mbili tukufu wampa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha mkarimu wa Ahlulbait Imamu Hassan (a.s)…

Maoni katika picha
Nyoyo zenye huzuni na machungu makubwa Alasiri ya Juma Tano ya mwezi (7 Safar 1440h) sawa na (17 Oktoba 2018m) zimefanya matembezi ya pamoja ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mkarimu wa Ahlulbait na Imamu wa pili miongoni mwa Maimamu wa uongofu baada ya Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Maukibu hiyo iliyo kua imetanguliwa na jeneza la kuigiza ilianzia katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ikapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakati wa matembezi yao waliimba kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na kubainisha ukubwa wa msiba huu katika nyoyo za waumini, walipo wasili katika uwanja wa haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), walipokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza ambayo walisoma kaswida ma mashairi yaliyo elezea dhulma alizo fanyiwa Imamu Hassan Aljtaba (a.s) na mambo yaliyo fanywa na viongozi waovu wa zama zake hadi kufikia kumuua kwa sumu akiwa ni mtu mwenye kufanya subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Kumbuka kua wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani hukumbuka tukio la kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika siku ya mwezi (7 Safar) siku aliyo kufa kwa sumu na akazikwa katika makaburi ya Baqii huko Madina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: