Kua miongoni mwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya milele ya Arubainiyya…

Maoni katika picha
Kwa kuzingatia kauli ya kiongozi wetu Imamu Abu Muhammad Hassan Askariy (a.s) isemayo: (Alama za muumini ni tano: kuswali rakaa hamsini na moja, ziara ya Arubaini, kuvaa pete kwenye mkono wa kulia, kugusisha uso chini na kudhihirisha bismillahi rahmaani rahiim -wakati wa swala-).

Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka mashariki na magharibi ya ardhi, wale washio mbali na ardhi tukufu ya Twafu watakao shindwa kuja kufanya ziara ya Arubaini ya bwana wa vijana wa peponi na ndugu yake pamoja na watoto wake na maswahaba wake watukufu (a.s), wajisajili majina yao kwa ajili ya kufanyiwa ziara kwa niaba.

Mtandao umeandaa watu watakao fanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kusoma dua maalumu kwa kila atakae sajili jina lake katika ukurasa wa ziara kwa niaba.

Kumbuka kua idadi ya watu walio jisajili na wakafanyiwa ziara katika msimu wa mwaka jana ilikua ni zaidi ya watu laki moja (100,000) kutoka kote duniani, na miongoni mwa walio wafanyia ziara kwa niaba ni wakili (mwakilishi) wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ambaye ni kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na jopo la wanachuoni watukufu waliokua ni wageni wa Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: