Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi, ambaye aliongeza kua: “Hakika vituo hivyo vitafanya mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:
- 1- Kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu, hasa sura zinazo somwa mara nyingi katika swala za faradhi za kila siku.
- 2- Kujibu maswali na kufafanua mambo yanayo husu Qur’ani.
- 3- Kuendesha kisomo cha Qur’ani tukufu katika kila sehemu ya kituo.
- 4- Kugawa folda zenye nyaraka zinazo elezea ziara na mambo yanayo husu Qur’ani”.
Akaendelea kusema: “Hakika Maahadi na matawi yake imepanga kuweka vituo hivyo katika mikoa ya Muthanna, Baabil, Najafu pamoja na Karbala tukufu, kwenye barabara kuu zinazo elekea Karbala, miongoni mwa barabara hizo ni: (barabara ya Karbala, Bagdad / Karbala, Baabil / Karbala, Najafu), vituo hivyo vitaendeshwa na wasomi kutoka katika matawi ya Maahadi ya mikoa hiyo, fahamu kua jambo hili linafanywa kwa mwaka wa nne mfululizo kwenye miji hiyo”.