Ushuhuda katika njia ya pepo: Watu wenye shauku kubwa ya kuuona mji wa Karbala wanandelea kupiga hatua kuelekea huko…

Maoni katika picha
Hawa hapa wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) wanaukaribia kidogo kidogo mji mtukufu wa Karbala, wanatembea kwa miguu kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), nyoyo zao zimesha wasili katika kaburi tukufu kabla ya miili yao, hakuna sauti inayo sikika kwao zaidi ya sauti ya Hussein, wala hakuna jina linalo itwa zaidi ya jina la Hussein, nyoyo zao zipo pamoja na yeye (a.s), wamebeba bendera za aina moja, macho yao yanatoka machozi kwa kwenda kukutana na mpenzi wao, hawajui maana ya uchovu wala hawaoni tabu yeyote katika kutembea kwao.

Katika mazingira haya ya Arubaini utaona mawakibu za Husseiniyya zinatoa huduma muda wote kwa watu wanaokwemda kumzuru Hussein kutoka kila kona ya dunia, zinawapa kila aina ya huduma ndogo na kubwa, fahari yao ni kutoa huduma, bali wamelelewa hivyo na wamerithi kutoka kwa mababu na mababu, huku mazingira yao yakisema: Hivi tumetekeleza ewe mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu?.

Utamkuta mzee, mtoto, kijana, bibi wote wananyoosha mikono kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) nawao kuja katika ardhi ya Twafu, ziara ya Arubaini inaushuhuri wa aina mbili kuu: kwanza watu hupenda kutembea kwa miguu, pili mazingira makubwa sana ya ukarimu wa wairaq kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s).

Kamera ya mtandao wa kimataifa Alkafeel inashiriki matembezi haya na inakuletea baadhi za picha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: