Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya nadwa ya majadiliano ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s), majadiliano hayo yanafanyika chini ya anuani isemayo: (Mbinu za kijeshi za Imamu Hussein –a.s- utafiti katika maktal ya Abu Mukhnifu), mada hiyowasilishwa na mwalimu wa historia katika chuo kikuu cha Karbala Dokta Zamaan Abedi Alma’amuri, mbele ya jopo la wasomi wa sekula na wadau wa turathi za Karbala.
Nadwa hii inaingia katika orodha ya majadiliano la kila mwezi yanayo fanywa na kituo cha turathi za Karbala ambayo huratibiwa na kituo hicho, na yaliongozwa na mwalimu wa lugha ya kiarabu wa chuo kikuu cha Karbala Dokta Falahu Rasuul.
Mada ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni hatua za msafara wa Imamu Hussein (a.s) kutoka Maka hadi Karbala, pamoja na vituo alivyo kua akipumzika (a.s), alifafanua jinsi alivyo kua anachagua sehemu na namna alivyo tumia jografia ya ardhi na uchimbaji wa handaki, mzungumzaji alisisitiza kua: “Mambo yote hakuyafanya bure, bali alitumia mbinu makini za kijeshi kwa mujibu wa riwaya ya Abu Mukhnifu”.
Nadwa ilikua na mwitikio mkubwa na wahudhuriaji waliuliza maswali kwa wingi na kulikua na majadiliano mazuri ya kielimu ambayo yamewapa elimu kubwa na muhimu wahudhuriaji.