Kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu chakamilisha maandalizi yote ya kushiriki katika kubeba mazuwaru wa ziara ya Arubaini.

Maoni katika picha
Kitengo cha mitambo (magari) cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kushiriki katika kuwabeba mazuwaru wa Arubaini, maandalizi hayo yamehusisha kuyafanyia matengenezo magari yote yatakayo shiriki katika kazi hiyo, pamoja na kuandaa madereva na kuwapanga katika gari hizo kwa kufuata ratiba itakayo tangazwa baada ya kuanza kazi rasmi.

Rais wa kitengo cha mitambo Muhandisi Abduljawaad amebainisha kua: “Usafiri ni jambo muhimu na unahitajiwa zaidi na watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo matukufu ya Karbala wakati wa Arubaini, kutokana na idadi kubwa ya mazuwaru, tumejipanga kwa kuandaa gari nyingi pamoja na kuzifanyia matengenezo”.

Akaongeza kua: “Kitengo chetu kitawajibika kubeba mazuwaru kuanzia mahala tutakapo pangiwa, tumeandaa gari zenye ukubwa tofauti, ikiwa ni pamoja na gari za wagonjwa na za maji, kutakua na kituo kitakacho simamia utendaji wa gari zitakazo shiriki kubeba mazuwaru, pia tumeandaa gari maalumu la kubeba mafundi watakao kua tayali kutengeneza gari lolote litakalo haribika likiwa kazini”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: