Mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma zakamilisha maandalizi na baadhi yake zimesha anza kutoa huduma…

Maoni katika picha
Kama kawaida ya kila mwaka, mawakibu Husseiniyya za kutoa huduma zilizo kuja Karbala pamoja na zile za hapa Karbala zimekamilisha maandalizi yao, zipo tayali kuwahudumia mazuwaru wanaokuja kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini.

Baada ya maukibu hizo kukamilisha maandalizi ya kiofisi na kiidara yanayo simamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na uongozi wa polisi wa mkoa wa Karbala, walianza kujenga mabanda na kuandaa sehemu za kutolea huduma, kila moja kwenye sehemu iliyo pangiwa, ambazo ni sehemu za njia kuu zinazo ingia na kutoka Karbala.

Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hutumia uwezo wao wote kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru, utawakuta wamevaa nguo nyeusi wako bize na kuandaa chakula pamoja na maandalizi mengine kwa ajili ya kutoa huduma bure kwa mazuwaru, wanategemea thawabu kutoka kwa Mola wao na wanatafuta radhi zake kwa utukufu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), sehemu kubwa ya mawakibu hizo zimesha anza kutoa huduma, ukizingatia kua mazuwaru wamesha anza kuwasiri, utawakuta watoto kwa wazee wanaume kwa wanawake wanashindana kutoa huduma bora kwa mazuwaru, wanatoa chakula, vinywaji, malazi pamoja na huduma zingine, huendelea hivyo hadi mwezi ishirini Safar, na wengine huendelea baada ya tarehe hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: