Haya ndio yaliyo husiwa na Marjaa Dini mkuu kwa mazuwaru na mawakibu zinazo toa huduma na za kuomboleza katika ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa maelekezo na nasaha kwa mazuwaru wa Arubaini na watumishi wa mawakibu za kutoa huduma na za kuomboleza pamoja na vyombo vya usalama, ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (9 Safar 1440h) sawa na (19 Oktoba 2018m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, vifuatavyo ni vipengele muhimu alivyo husia:

  • - Ziara ya Arubaini ni sehemu ya kuonyesha mapenzi na kuhuisha ahadi kwa bwana wa mashahidi (a.s).
  • - Ziara ya Arubaini ni kuhuisha ahadi na kuenzi malengo yaliyo sababisha Imamu Hussein (a.s) apambane hadi kufa.
  • - Kujenga undugu kwa mtu mmoja mmoja na vikundi ni faida kubwa inayo patikana katika ziara hii.
  • - Kuendelea kufanyika ziara hii kila mwaka hilo ni jambo tukufu na lakujivunia.
  • - Watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein (a.s) ni sawa na wanaitikia wito wake pale alipo sema (Je! Kuna wa kuninusuru aje aninusuru?).
  • - Matembezi haya ni matembezi ya huzuni kwa sababu yanatukumbusha msiba, lakini pia ni matembezi matukufu kwa kua yanatukumbusha malengo aliyo kuwa nayo bwana wa mashahidi (a.s).
  • - Matembezi haya ni kielelezo cha mafanikio.
  • - Yatupasa kuendeleza matembezi na ziara ya Arubaini kwa sababu yanaonyesha mafungamano makubwa na bwana wa mashahidi (a.s).
  • - Kuna watu wanahaki ya kuenziwa na haifai kuwapuuza bali ni watu wa kujifaharishia.
  • - Watu walio fanikiwa kuja ziara wanatakiwa wawaombee watu ambao hawakujaliwa kuja.
  • - Vijana wanatakiwa wakumbuke kua walikua wanatembea na rafiki zao kila mwaka na sasa rafiki zao hao wamesha fariki.
  • - Vijana hoa hawajaishi sana hapa Duniani, lakini walikua na imani madhubuti na mapenzi makubwa ya Dini yao pamoja na taifa lao na wakafaulu kwa kupata shahada tukufu zaidi.
  • - Inatakiwa kuthamini mchango wa wahisani wa mawakibu pamoja na juhudi kubwa na mali wanazo jitolea kwa ajili ya ziara.
  • - Pia kuna walio jitolea mali na nafsi zao kwa ajili ya mazuwaru.
  • - Watu hao wamelea nafsi zao na za watoto wao katika utowaji, unapofika wakati wa kujitolea hawaogopi chochote bali wapo tayali kujitolea hadi damu zao, na jambo hili ni miongoni mwa baraka za mawakibu hizi na kumtumikia bwana wa mashahidi.
  • - Imamu Hussein (a.s) ndiye wa kushukuriwa katika jambo hili na mawakibu pia lazima tuzishukuru kwa kila zuri wanalo fanya.
  • - Yatupasa kuzishukuru mawakibu kwa malezi mazuri na kulinda utamaduni mwema pamoja na kuakisi picha nzuri ya watu wa Imamu Hussein (a.s).
  • - Riwaya zinazo shajihisha kumzuru Imamu Husein (a.s) zinathibitishwa na mazuwaru pamoja na wahudumu wa mawakibu hizi.
  • - Tunatakiwa kuwapongeza, kwa hakika wanastahiki pongezi katika kila kitu hadi katika uadhimishaji wao.
  • - Muumini huwa na mazingatio kila anapo tajwa Imamu Hussein (a.s).
  • - Mawakibu hizi lazima ziwe na muonekano wa huzuni katika utendaji wao na uadhimishaji wao.
  • - Roho ya Husseiniyya inatakiwa ionekane kwa yule anayefanya maombolezo.
  • - Lazima huzuni iambatane na unyenyekevu, jambo hilo hutokea kimaumbile.
  • - Inabidi kulinda mazingira ya uliaji na kuhuzunika, hakika ziara ya Arubaini sio sawa na ziara zingine.
  • - Ziara ya Arubaini imejengeka katika misingi ya msiba, tunaomba yafanyike mambo yanayo stahiki katika ziara hii.
  • - Tunasisitiza umakini na kuchukua tahadhari za kiusalama, na vyombo vinavyo husika viweke ulinzi zaidi katika mawakibu.
  • - Mtu aliyeshindwa katika uwanja wa vita hufanya jinai za kushambulia makundi ya watu wasio na hatia, tunatakiwa kuwa makini wakati wote na kuchukua tahadhari.
  • - Nakuombeni muwe makini na muwe na tahadhari, pia mjiepushe kutembea katika barabara zinazo pita gari, na madereva jiepusheni na mwendo kasi.
  • - Kila mwaka wanachuoni na wanafunzi wa hauza hujitolea kuwahudumia mazuwaru, nawaomba mazuwaru wanufaike na uwepo wao.
  • - Baadhi ya watu huona aibu kuuliza, aibu hiyo haifai.
  • - Ulizeni sana maswali, wao wapo tayali kuwajibu na hiyo ndio furaha yao.
  • - Usiache kuuliza swali lolote la kisheria au hata lisilokua la kisheria, ni fursa nzuri kwa mtu kujifunza mambo ya Dini yake anapo kuja kwa bwana wa mashahidi (a.s).
  • - Imamu Hussein (a.s) ndio mwalimu wetu wa milele na milele na ataendelea kua mwalimu wetu daima Insha-Allah.
  • - Pia kuna wakina dada ambao wapo tayali kujibu maswali ya wakina mama wanaokuja ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: