Shirika la reli: Tumeandaa treni 24 kwa ajili ya kubeba mazuwaru wa ziara ya Arubaini na hilo ni jukumu letu…

Maoni katika picha
Shirika la reli limetangaza kua limeandaa treni 24 kwa ajili ya kubeba mazuwaru wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), treni hizo leo zimeanza kazi rasmi kutokea katika stesheni nne.

Taarifa hiyo imetolewa na msemaji mkuu wa shirika la reli Abdusataar Muhsin kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel, ambapo amesema kua: “Uongozi wa shirika la reli umetenga treni 24 kwa ajili ya kubeba mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kutoka katika mikoa ya kati na kusini hadi Karbala, uongozi unatumia asilimia kubwa ya treni zake zikiwemo na treni za uturuki”.

Akaendelea kusema kua: “Treni hizo zimeanza kazi rasmi siku ya Juma Mosi (20 Oktoba 2018m) sawa na (10 Safar 1440h) kutoka katika stesheni nne, ambazo ni Bagdad hadi Karbala, Basra hadi Karbala, na kutoka soko la wazee (suuq shuyuukh) na Diwaniyya hadi Karbala, safari zote zina punguzo kubwa la bei”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: