Miji ya mazuwaru na majengo ya kutolea huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Idara ya miji ya mazuwaru na majengo ya kutolea huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kua ipo tayari kuwapokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), wamesha kamilisha matengezo yote ya lazima chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Ataba tukufu, na sasa wapo tayali kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu wa Arubaini.

Mgawaha (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya wa nje uliopo katika barabara ya (Najafu – Karbala) umetangaza kua uko tayali kuanza kutoa huduma, na tayali umesha anza kutoa hutuma siku chache zilizo pita. Hali kadhalika majengo mengine ya kutoa huduma kama vile: jengo la Alqami lililopo katika barabara ya (Baabil – Karbala), jengo la Ummul Banina (a.s) lililopo katika barabara ya (Najafu – Karbala), jengo la Shekh Kuleini (r.a) lililopo katika barabara ya (Bagdad – Karbala), yametangaza kua yapo tayali kupokea na kuwahudumia mazuwaru ambao mwaka huu wanatarajiwa kuwa wengi zaidi ya mwaka jana, miongoni mwa maandalizi waliyo fanya ni:

  • 1- Kuandaa kumbi zote kwa ajili ya malazi na kutolea huduma.
  • 2- Kuandaa idadi kubwa ya nguo za kujifunika (mablangeti) na matandiko.
  • 3- Kukarabati barabara zote zinazo ingia katika majengo hayo.
  • 4- Kupanda miti katika majengo hayo (kuweka mandari nzuri za bustani zake).
  • 5- Kuandaa vyakula na kuvigawa kwa mazuwaru.
  • 6- Kuweka sehemu za hakiba kwa ajili ya kupokea mazuwaru katika siku za kilele cha ziara na kuziwekea mahitaji yote ya lazima.
  • 7- Kufungua vituo vya afya kwa kushirikiana na vitengo husika katika sekta hiyo.
  • 8- Kukarabati njia za maji pamoja na bafu zote na kuweka kila kinacho hitajika.
  • 9- Kukarabati viyoyozi vyote.
  • 10- Tumewasiliana na kamati inayo husika na watu wanaojitolea kwa ajili ya kupewa wahudumu wa kutosha katika majengo hayo.
  • 11- Tumekarabati njia zote za umeme na mitambo ya zima moto na vinginevyo.

Kuna mambo mengine mengi tuliyo fanya nafasi haitoshi kueleza kila kitu, pia tumeandaa vyoo vya dharura tulivyo viweka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, hatujafanya kazi ya maandalizi katika majengo hayo peke yake, bali tumeandaa sehemu zingine kwa ajili ya kupumzika mazuwaru na kuwapa huduma kwenye shule husseniyya zilizo andaliwa kupokea mazuwaru, pamoja na vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya pia vitatumika kutoa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: