Matangazo ya Arubainiyya ya 1440h: Mazuwaru wanao kwenda Karbala kutoka katika mikoa ya kusini…

Maoni katika picha
Bado mamilioni ya watu wanaendelea kumiminika katika mji wa Karbala tukufu kutoka katika mikoa ya kusini, kituo kikuu inapo anzia misafara hiyo ni katika mji wa Basra kwa ajili ya kwenda kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), misafara hiyo ilianza kabla ya siku tisa za nyuma, mwandishi wa mtandao wa kimataifa Alkafee ametuhabarisha kuhusu matembezi hayo kua:

  • 1- Mkoa wa Basra umebaki mtupu, hakuna wageni wanaokaa katika mkoa huo wala mwenyeji, wengi wamekwenda katika mawakibu na vikundi vya kutoa huduma katika miji mbalimbali na katika mji wa Karbala.
  • 2- Mipaka ya mkoa wa Dhiqaar inashuhudia ongezeko kubwa la mazuwaru, kuna idadi kubwa ya watu ambao wamejiunga na misafara ya mazuwaru, sambamba na idadi kubwa kuweka kambi katika barabara zinazo tumiwa zaidi na mazuwaru kwa ajili ya kutoa huduma.
  • 3- Eneo lenyo mazuwaru wengi sana ni baina ya Naswiriyya, Samawa na Ramitha.
  • 4- Siku ya Juma Mosi ilitoka maukibu kubwa ya watu wa Samawa ambayo ilionekana kuwa maukibu kubwa zaidi katika mkoa wa Muthana.
  • 5- Mikoa mingine kama vile Misaani, Diwaniyya na Waasit inamazuwaru wa kawaida.

Akasema kua: “Vyombo vya ulinzi na usalama na vikosi vya Hashdi Sha’abi vimeimarisha ulinzi kwa mazuwaru watukufu, pia idara za utumishi na afya zimeandaa vituo vinavyo hamishika kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru”.

Akaongeza kua: “Mazuwaru wanania kubwa ya kufanya ibada hii pamoja na ugumu wa hali ya hewa”, akasema: “Kuna idadi kubwa ya watu waliokuja kushiriki katika matembezi haya kutoka nchi jirani, matembezi yaliyojaa watoa huduma wa kujitolea kwenye barabara zote kubwa na ndogo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: