Kuna ishara ya kuongezeka kwa kiwango kibubwa cha mazuwaru wa Arubaini mwaka huu, mapema mwezi huu idadi kubwa ya mazuwari wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) imeanza kuwasiri katika mji wa shahada na kujitolea Karbala tukufu, watu wanaingia kwa wingi toka siku nne za nyuma kupitia barabara ya Najafu na Hilla, leo na jana idadi imeongezeka zaidi kwa kuanza kuingui makundi kwa makundi ya watu wakati hapo awali walikua wanaingia mmoja mmoja, wote hao wanalengo moja kuu la kupata baraka za Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mawakibu na vibanda vya kutoa huduma vimeenea katika barabara zote zinazo ingia na kutoka Karbala, sawa ziwe za wakazi wa Karbala au zilizo kuja kutoka mikoa mingine ya Iraq ambazo zilifika mapema na kufanya maandalizi ya kuwahudumia mazuwaru watukufu, wamejipanga na wako tayali kutuo huduma kwani ni jambo walilokua wakilisubiri kwa hamu mwaka mzima.
Maukibu hizo hutoa chakula, vinywaji pamoja na kuandaa sehemu maalumu za kupumzikia mazuwaru, wamejenga mabanda ya kutolea huduma na wamefungua husseiniyya mbalimbali bila kusahau walio fungua nyumba zao za kuishi kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kugawa chukula nyakati zote tatu.
Kwa upande mwingine Ataba tukufu za Karbala zinatumia uwezo wao wote kwa ajili ya kuhakikisha zinatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru, bila kusahau idara za serikali na za ulimzi na usalama hali kadhalika idara ya afya, maji na zinginezo.