Kama kawaida yake kwenye kila msimu wa Arubainiyya, umeondoka msafara mkubwa wa watu wa Samaawa kuelekea Karbala, kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), jambo hilo limezoweleka kwa miaka mingi, matembezi hayo huambatana na igizo linalo onyesha mambo waliyo fanyiwa mateka wa Ahlulbait (a.s), kuanzia mauwaji ya Twafu na yaliyo jiri baada ya mauwaji hayo, matembezi haya hupewa umuhimu mkubwa na watu wengi husubiri ili washiriki katika matembezi haya, hufanywa maigizo yanayo onyesha namna mateka walivyo pelekwa Sham na walivyo rudishwa mwezi ishirini Safar.
Mwandishi wa mtandao wa Alkafeel anaye shiriki katika matembezi hayo akiwa katika mkoa wa Muthanna ametuambia kua: “Hakika mkoa huu kwa sasa unapokea idadi kubwa sana ya watu wanaokwenda ziara Karbala chini ya ulinzi mkali na huduma bora, huduma zimeongezwa zaidi na watu waliokuja kutoka mikoa ya kusini, hakika matembezi haya yanakumbusha harakati ya Imamu Hussein (a.s) ambayo itaendelea kukumbukwa milele na milele”.
Mwakilishi wa mawakibu katika mkoa wa Muthanna chini ya kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Saadi Rahim Abadali amesema kua: “Malaki wa watu wa Samaawa wameanza kutembea kuelekea Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), matembezi haya yatakua na vituo vingi katika miji ambayo msafara huo unapita hadi kufika Karbala, na huu ni mwaka wa kumi na moja ambao matembezi haya yanafanyika ya kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na jambo hili ni dogo sana ukilinganisha na namna Imamu alivyo jitolea na madhila aliyo fanyiwa na watu waovu Yazidi na vibaraka wake”.
Kwa upande mwingine askari wa Muthanna wameimarisha ulinzi, katika matembezi haya pia wameshiriki watu wa mikoa ya kusini walio penda kuungana na ndugu zao katika matembezi haya ya kuomboleza.