Kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika ziara ya Arubainiyya na kuweka mazingira ya amani kwa mazuwaru ikiwa ni pamoja na kuziba mianya inayo weza kutumiwa na watu wanaotaka kuvuruga amani ya ziara, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinafanya ukaguzi mkali na kimeimarisha ulinzi katika jangwa la magharibi ya mkoa wa Karbala na upande wa mkoa wa Ambaar kwa kushirikiana na kikosi cha Furaat Ausatu na kikosi cha muungano (Itihadi) pamoja na askari wa Karbala, program hii imepewa jina la “Shihaab” ambayo ni program maalumu ya kuziba mianya inayoweza kutumiwa na magaidi wa Daesh.
Wasimamizi wa program hii kutoka katika kikosi cha Abbasi wamebainisha kua; vikosi vya wanajeshi vikiongozwa na kikosi cha vifaru pamoja na kikosi cha anga sambamba na vikosi vingine vitatu pamoja na vikosi vingine maalumu wameimarisha ulinzi katika jangwa la upande wa magharibi ambalo magenge ya magaidi hulitumia kama kichaka.
Akaongeza kua: Hii ni program maalumu ya kuimarisha ulinzi katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuulinda mkoa mtukufu wa Karbala katika upande wa magharibi.
Kazi zote za ulinzi zinafanywa chini ya ushirikiano wa makamanda kikosi cha Furaat Ausatu.