Kwa mara ya kwanza baada ya kukombolewa ardhi yao kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh: Watu wa Mosul wanakuja kuhuisha ahadi yao kwa kiongozi wao Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Ni matembezi waliyo yakosa katika miaka ya nyuma, baada ya kukimbia nyumba zao na kutengana na familia zao kutokana na vita, leo baada ya kukombolewa mji wao wanakuja wakiwa na shauku kubwa ya kuliona kubba la bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ndio. Watu wa Mosul, Tal-Afar, Sahal-Nainawa pamoja na miji mingine wanakuja kuhuisha ahadi zao kwa Hussein (a.s) wakiwa wamenyanyua bendera za mazingatio na shukrani pamoja na heshima kubwa ya damu zilizo mwagika katika kukomboa miji yao iliyo kua imetekwa na magaidi wa Daesh, wakiwa na bendera za Hashdi Sha’abi watukufu, pia ikiwa kama sehemu ya Hashdi Sha’abi kukamilisha mafanikio waliyo pata, nao wameshiriki pamoja na makundi ya waombolezaji wa Husseiniyya, kwa hiyo pendera za kwanza zinazo pepea ni za Imamu Hussein (a.s) na za pili ni bendera za Hashdi Sha’abi watukufu.

Leo hakuna kitu cha kuwazuwia, pamoja na urefu wa safari watakayo tembea hadi Karbala lakini hilo sio tatizo kwao kutokana na ukubwa wa shauku waliyo nayo ya kufanya ziara ya Arubaini, wanatembea kwa moya mmoja wakitambua kuwa wanakwenda kwa mjukuu wa Mtume aliye uwawa kikatili kwa kuchinjwa.

Tunapenda kufahamisha kua watu wa Mosul na miji ya jirani yake walikosa fursa ya kwenda ziara kwa kutembea kutokana na miji yao kuvamiwa na magaidi wa Daesh waliyo fanya mauwaji wa kinyama na kusababisha wakazi wa miji hiyo wakimbie kabla ya kuwafurusha na kuirudisha katika udhibiti wa taifa kwa juhudi za majemedari wa fatwa tukufu ya kujilinda na kujitolea kwao kutukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: